Magonjwa ya ngozi hili ni tatizo sugu kwa watumiaji hasa wa muda mrefu wa vipodozi kwani husababisha kuungua. kuvimba, kuharibika na kutoka vipele kwenye ngozi ambayo huchukua muda mrefu kutibika au kutotibika kabisa.
Muwasho na Allergy hii huweza kuathiri ngozi, maskio, tumbo na mifumo wa upumuji na fahamu kutokana na harufu kali au kemikali zilizopo katika vipodozi hivyo kumpasa mtumiaji kuwa makini na uchaguzi wa vipodozi.
Uharibifu wa viungo na umbo kama macho, pua midomo, makalio, maskio pua hasa kwa wale wanaotumia lenzi zenye kemikali, heleni mdomoni na kwenye ulimi au silva na dhahabu katika meno.
Kuharibika kwa kucha. hii ni kwa wale wanaotengeneza kucha saluni kwani huongeza urembo na hupoteza ubora wa kucha katika rangi, urefu na upana na kuzifanya dhaifu sana na huweza kung'oka kirahisi
Saratani na magonjwa sugu hii husababishwa sana na kemikali zilizo katika vipodozi. mfano lipsticks zina kemikali zinazozababisha upungufu wa damu(Anemia). Pia vipodozi vingi vina kemikali ambazo hupunguza kinga ya mwili na kusababisha magonjwa sugu ya moyo, figo na ini.
Kuzeeka kwa ngozi, vipdozi vingi husababisha baadhi ya watu kuwa na ngozi zenye mikunjo na kuzeeka pale anapoaacha kutumia.
Matatizo ya uzazi, matumizi ya muda mrefu vipodozi husababisha kansa ya uzazi kwa jinsia zote au kuharibu mfumo wa uzazi na hivyo kusababisha utasa na ugumba.
Maumivu ya kichwa na mabega, watu wengi hupata maumivu ya kichwa, mabega, mgongo sambamba na uchovu, kichevuchevu au kutapika au kupoteza fahamu na msongo wa mawazo pale wanapotumia vipodozi kwa muda mrefu.

Hata hivyo sio kwamba vipodozi vyote huleta madhara bali madhara hayo utokana na matumizi na aina ya vipodozi vinavyotumika hivyo ni muhimu kupata ushauri kabla ya matumizi, kuacha au kutumia vipodozi vya asili.
KWA MSAADA ZAIDI BONYEZA HAPA AU ACHA COMMENT YAKO CHINI
No comments:
Post a Comment