Ripoti mpya inasema Mwanamke mmoja wa Kenya amefia kwenye uwanja wa ndege Jomo Kenyatta Nairobi kwa tetesi kwamba alikua anaumwa Ebola au Marbug ambapo familia yake imeilaumu Serikali kwa kifo cha ndugu yao kwa kutelekezwa na wauguzi kwenye Clinic ya uwanja wa ndege waliokua na hofu ya kuambukizwa ugonjwa wa Ebola.
NTV Kenya wameripoti kwamba Marehemu ambae alikua mfanyabiashara aliondoka nchini Kenya na kuelekea Juba Sudan ambapo alipitia Uganda wakati mlipuko wa Marburg ulipotokea na alipowasili Juba alikua anavuja damu kwenye sehemu ya uzazi jambo lililofanya dada yake amrudishe Nairobi kwa ajili ya matibabu.
Mama Wanjiku pamoja na rafiki yake pamoja na Marehemu waliwekwa kwenye chumba kimoja kwa zaidi ya saa tano kabla ya kuruhusiwa kuondoka ambapo Wanjiku alifariki dunia akiwa kwenye kiti cha magurudumu.
Mama mzazi na rafiki yake waliruhusiwa kuondoka kabla ya matokeo ya uchunguzi wa matibabu kutolewa, kama Marehemu alikua akiugua Ebola au Marburg basi kuachiliwa kwao kungepelekea kusambaa kwa ugonjwa huo kwa haraka….
BOFYA HAPA KUSIKIA SAUTI
No comments:
Post a Comment