Mtoto huyo anayefahamika kwa jina la Fidel Odinga alikutwa akiwa amefariki dunia kitandani kwake asubuhi ya leo (jumapili) baada ya kurudi nyumbani kwake alfajiri akiwa anatoka kukutana na rafiki zake .
Mara ya mwisho Fidel aliripotiwa kukutana na baba yake usiku wa jumamosi kabla ya kuagana na kwenda kukutana na rafiki zake katika sehemu ambayo haijawekwa wazi na baada ya hapo alirudi nyumbani kupumzika hadi mauti yalipomkumba .
Mwili wa Fidel Odinga ulikutwa kitandani kwake baada ya kurudi nyumbani alfajiri akiwa anatoka kukutana na rafiki zake .
Fidel ameacha mke mmoja na mtoto mmoja mwenye umri wa miaka miwili ambaye alizaa na mke wake Getachew Bekele ambaye ni raia wa Eritrea .
Saa chache baada ya habari za kifo cha Fidel makundi tofauti ya watu yalianza kufanya maandamano na vurugu maeneo ya Ngong nje kidogo ya Jiji la Nairobi wakipiga kelele za ‘Nani amemuua Fidel’ wakimaanisha kuwa kifo chake kimesababishwa na mtu huku wakishindwa kutaja sababu au chanzo kamili
No comments:
Post a Comment