Madaktari na waalamu wa afya wanashauri kulala bila nguo za ndani wakati wa usiku ili kuwezesha viungo vya uzazi kupata hewa ya kutosha ili kuepuka maambukizi ya fangasi na kutoa harufu mbaya katika sehemu za siri. Kuvaa nguo za ndani wakati wa kulala usababisha kubana sehemu za siri na joto kupita kiasi ambayo usababisha joto kupita kiasi na unyevu na kuvutia ukuaji wa fangasi na bakteria kwa jinsia zote huku pia zikisababisha upungufu wa mbegu za kiume na harufu mbaya.
Wednesday, 3 September 2014
Tuesday, 2 September 2014
KAMA UNASUMBULIWA NA MAUMIVU YA MGONGO
Maumivu chini ya mgongo hutokea sana kwa kila mtu na mara nyingi huwa ni chini ya mbavu za nyuma na juu ya miguu na huweza kusambaa mpaka kwenye kiuno na hips. Maumivu haya usikika na kuumiza pale unapoinua kitu, kusimama, kukaa kwenye kiti au kutembea na usababishwa na matumizi kupita kiasi ya misuli, kano, mishipa na neva za mgongoni au kwenye pingili za uti wa mgongo kutokana na kugandamizwa sana. Pia huweza kusababishwa na kuvunjika au maambukizi katika pingili za uti wa mgongo, umri mkubwa, saratani ya mifupa,uzito kupita kiasi mawe katika figo, uvimbe na saratani ya kizazi .
KAMA UNASUMBULIWA NA KIUNGULIA MARA KWA MARA
UMUHIMU WA KUOTA JUA ASUBUHI
Watu wengi huwa na upungufu wa vitamini D kwasababu hawatoki nje kupata mwanga wa jua ambao huchochea seli katika ngozi ya mwili wako kuzalisha Vitami D inayoboresha afya ya mifupa na meno na kukukinga na hatari ya kushambuliwa na magonjwa ya moyo, kisukari na saratani.
MAMBO YANAYOSABABISHA UPUNGUFU AU UKOSEFU WA MBEGU ZA KIUME
Ni vigumu sana kugundua dalili na ishara za ukosefu au upungufu wa mbegu za kiume kwani tendo la ndoa uendelea kufanyika kawaida na kutoa shaawa zisizokuwa na mbegu za kiume au zenye upungufu ambazo usababisha utasa kwa wanaume. Yafuatayo ni mambo ambayo huweza kusababisha tatizo ili na kumfanya mweza akose ujauzito kwa muda mrefu.
JINSI YA KUTUNZA NGOZI ZENYE MAFUTA
Ngozi
yenye mafuta kwa kawaida huwa inang'ara, nene na yenye rangi
iliyotitia. Mara nyingi ngozi yenye mafuta mengi sana huwa na chunusi
nyingi na vipelepele na mara nyingine huwa na chunusi zenye vichwa
vyeusi. Katika aina hizi za ngozi mafuta hutokana na tezi za sebaceous
na kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango kinachotakiwa. Mafuta hayo husambaa
katika ngozi na kuifanya iwe na mafuta mafuta.
Monday, 1 September 2014
TATIZO LA KUTOKWA NA DAMU KWENYE FIZI
Mara nyingi kuvimba au kutokwa na damu kwenye fizi huweza kusababishwa na magonjwa mbalimbali ya kinywa na meno ambayo husababishwa na kutofanya vizuri usafi wa meno kwa usahihi au maambukizi ya bakteria ambao usababisha utando mgumu kwenye meno. Utando huu hauwezi kutolewa kwa kupiga mswaki bali kwa kutumia vifaa maalumu na wataalamu wa meno. Pamoja na maambukizi au kutofanya usafi pia kutokwa na damu kwenye fizi usababishwa na magonjwa ya damu, kupiga mswaki kwa nguvu, ukosefu wa vitamini C na K.
Subscribe to:
Posts (Atom)
