Saturday, 29 March 2014
SABABU ZA KUTOKA HARUFU MBAYA UKENI NA NAMNA YA KUJIKINGA
Wanawake na watu wengi huzani kuwa harufu mbaya itokayo ukeni ni matokeo ya uchavu na kutojisafisha vizuri… Matokeo yake huongeza jitihada katika kujisafisha bila mafanikio ya kuondokana na tatizo hili… Kihalisi, badala kusuluhisha, unapojisafisha zaidi ni unaongeza tatizo badala ya kutatua… Japokuwa ni kweli mara nyingine inaweza ikawa ni sababu ya uchafu… Ila mimi naamini walio wengi huwa wanazingatia usafi… Ndo maana nimeona leo tupeane mawazo juu ya tatizo hili, na kujua namna ya kujikinga
VSABABISHI
i. Bacteria
Wednesday, 26 March 2014
Tahadhari kuhusu ugonjwa wa dengue nchini
Kutoka GAZETI LA MWANANCHI
Dar es Salaam. Wananchi wameaswa kuchukua hadhari juu ya ugonjwa wa dengue ambao dalili zake ziko sawa na zile za malaria.
Dar es Salaam. Wananchi wameaswa kuchukua hadhari juu ya ugonjwa wa dengue ambao dalili zake ziko sawa na zile za malaria.
Mpaka sasa ugonjwa huo hauna tiba maalumu wala
chanjo na njia pekee ya kukabiliana nao ni kutambua dalili zake kama
vile homa, kupungukiwa maji au damu, kuumwa kichwa, maumivu ya viungo na
uchovu. Mgonjwa anaweza kupoteza maisha endapo atachelewa kupatiwa
matibabu.
Monday, 24 March 2014
FAIDA YA KULA NDIZI KWA WAGONJWA WA MOYO NA FIGO
Kula ndizi, ni muhimu sana kwa afya zetu kwani husaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo na mishipa ya damu kama myocardial infarction, kiharusi na kudhibiti shinikizo la damu.
soma na hii:>>>>MAGONJWA HATARI YANAYOTIBIWA NA MBEGU ZA MABOGA
Pia ndizi huweza kuzuia matengenezo ya vidonda vya tumbo na duodenal ulcer pamoja na kuzuia homa na kuzeeka kwa ngozi kutokana na kuwa na vitamini C na E.
Aidha Ndizi inapendekezwa kuwa ni mlo wa kila siku kwa ajili ya watu wanaosumbuliwa na magonjwa wa figo na moyo.
MAGONJWA 10 UNAYOWEZA KUJITIBU KWA KUTUMIA MBEGU ZA MABOGA:
ZIKIWA
zimesheheni protini na madini kadhaa kama vile chuma, kopa, maginizia,
manganizi na zinki, mbegu za maboga zinakuwa mbegu bora na muhimu
kutafuna kila wakati kama wewe ni mpenzi wa kutafuna-tafuna.
Imethibitika pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida lukuki
kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10:
01 UGONJWA WA MOYO:
Mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini aina ya maginizia (magnesium) ambayo huboresha utendaji kazi wa viungo vya mwili. Huimarisha usukumaji wa damu kwenye moyo, huimarisha ukuaji wa mifupa na meno, huifanya mishipa ya damu kupitisha damu kwa urahisi na hufanya upatikanaji wa haja kubwa kuwa laini.

02 KINGA YA MWILI:
Mbegu za maboga pia zina kiasi kingi cha madini ya Zinki (Zinc). Madini haya yana faida nyingi mwilini, ikiwemo kuimarisha kinga ya mwili, kuboresha ukuaji na uundaji wa chembechembe hai za mwili, kuboresha usingizi, kuboresha ladha mdomoni na harufu, huboresha afya ya macho na ngozi, hurekebisha sukari na huboresha nguvu za kiume pia.
Upungufu wa madini ya ‘Zinc’ mwilini una uhusiano mkubwa sana na matatizo ya kuzaa watoto njiti, kuota chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo darasani kimasomo na matatizo mengine mengi ya kimwili na kiakili.

03 MAFUTA YA OMEGA -3:
Omega-3 ni moja kati ya mafuta muhimu sana mwilini. Jamii ya karanga pamoja na mbegu za maboga ni miongoni mwa mbegu zenye kiasi kingi cha mafuta aina hii. Hivyo ulaji wa mbegu za maboga utakuwezesha kupata kirutubisho hiki muhimu katika mwili wako na kukupa faida za mafuta haya ambazo ni nyingi.

04 KIBOFU CHA MKOJO:
Tangu enzi za mababu zetu, mbegu za maboga zimetumika kuimarisha afya ya wanaume kutokana na kuwa na kiasi kingi sana cha madini aina ya Zinc ambayo ni muhimu sana kwa afya ya kibofu cha mkojo. Mbegu za maboga pamoja na mafuta yake, yote kwa pamoja hutoa kinga kwenye kibofu kupatwa na matatizo ya kiafya, yakiwemo yale ya saratani ya kibofu.

05 KINGA DHIDI YA SARATANI:
Imethibitika kwamba watu ambao hula mlo wenye kiasi kingi cha mbegu za maboga wamegundulika kuwa na hatari ndogo sana ya kupatwa na saratani za tumbo, matiti, mapafu na kibofu.
Imethibitika kwamba watu ambao hula mlo wenye kiasi kingi cha mbegu za maboga wamegundulika kuwa na hatari ndogo sana ya kupatwa na saratani za tumbo, matiti, mapafu na kibofu.
soma na hii: TIBA YA MAGONJWA MBALIMBALI KWA KUTUMIA ASALI
06 UGONJWA WA KISUKARI:
Utafiti uliofanywa kwa kuwalisha wanyama mbegu za maboga, umeonesha kuwa ulaji wa mbegu za maboga, husaidia kurekebisha kiwango cha ‘Insulin’ mwilini na hivyo kumuepusha mtu kupatwa na ugonjwa wa kisukari.

07 MATATIZO YA UKOMO WA HEDHI:
Mara nyingi kina mama watu wazima ambao wamefikia ukomo wa hedhi, hupatwa na matatizo mbalimbali yanayosababishwa na hali hiyo. Hata hivyo utafiti umeonesha kuwa mbegu za maboga zina uwezo wa kurekebisha hali hiyo na kuondoa kabisa matatizo ya kiafya yatokanayo na ukomo wa hedhi.

08 AFYA YA MOYO NA MAINI:
Mbegu za maboga, ambazo zina kiasi kingi cha mafuta mazuri, kamba lishe na virutubisho vinavyoimarisha kinga ya mwili (antioxidants), zimeonekana kuwa bora pia kwa afya ya moyo na ini, huweza kumpatia mlaji kinga dhidi ya matatizo ya kiafya katika moyo na ini.

09DAWA YA USINGIZI:
Mbegu za maboga zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha ‘homoni’ za usingizi. Ulaji wa mbegu za maboga saa chache kabla ya kupanda kitandani, hasa ukila pamoja na tunda lolote, kunasaidia kupata usingizi mzuri na tulivu.

10 DAWA YA UVIMBE:
Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa mbegu za maboga zina mafuta yenye uwezo wa kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya uvimbe (inflamatory diseases) sawa na dawa aina ya ‘indomethacin’, lakini mbegu hizi hazina madhara kama ilivyo kwa hiyo dawa.
JINSI YA KULA MBEGU ZA MABOGATafiti kadhaa zimeonesha kuwa mbegu za maboga zina mafuta yenye uwezo wa kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya uvimbe (inflamatory diseases) sawa na dawa aina ya ‘indomethacin’, lakini mbegu hizi hazina madhara kama ilivyo kwa hiyo dawa.
Ili kupata faida zake zote, zikiwemo zile za mafuta yake, inashauriwa kula mbegu hizo zikiwa kavu, bila kuzikaanga. Hakikisha pia unapata mbegu zilizohifadhiwa vizuri ambazo hazijaoza wala kuwa na fangasi. Iwapo utapenda kuzikaanga, basi hakikisha unazikaanga kwa muda usiozidi dakika 15, unaweza pia kuongeza chumvi kidogo kupata ladha, lakini za kukaanga zitakuwa hazina mafuta mengi kama zile kavu
Thursday, 20 March 2014
Jinsi Asali inavyoweza kukutibu matatizo mbalimbali
ASALI
inafahamika kwa muda mrefu
kama chakula muhimu ambacho pia
kinasaidia sana katika kupambana na
magonjwa mbalimbali na matatizo
yatokanayo na uzee.
Kwa mujibu wa tafiti mpya za
wataalamu wa madawa lishe na vifaa
tiba, imedhihirika kwamba, uwezo wa
asali kutibu unaweza kuongezeka
maradufu kama itachanganywa na
mdalasini.
kama chakula muhimu ambacho pia
kinasaidia sana katika kupambana na
magonjwa mbalimbali na matatizo
yatokanayo na uzee.
Kwa mujibu wa tafiti mpya za
wataalamu wa madawa lishe na vifaa
tiba, imedhihirika kwamba, uwezo wa
asali kutibu unaweza kuongezeka
maradufu kama itachanganywa na
mdalasini.
Madhara na Matibabu ya mba mwilini
Hali hii hutokana na uwezo wa fangasi kusimamisha shughuli za uzalishaji wa
homoni na kemikali inayoipa ngozi rangi yake. Hii husababisha upungufu wa
kemikali na hivyo mabadiliko ya rangi ya ngozi.
Je, ni vipi hushambulia ngozi?
Maeneo yenye mabaka yanayoletwa na fangasi wa aina hii hubadilika rangi yake na kuwa na rangi hafifu au inayoonekana zaidi (kama ni mtu mwenye rangi ya maji ya kunde basi ngozi iliyoathiriwa hubadilika na kuwa nyeupe au nyeusi sana.
Hali hii hutokana na uwezo wa fangasi wa aina hii kusimamisha shughuli za uzalishaji wa homoni na kemikali inayoipa ngozi rangi yake. Hii husababisha upungufu wa kemikali na hivyo mabadiliko ya rangi ya ngozi.
Upungufu huo ya rangi ya ngozi si wa kudumu, bali ngozi hurudi kwenye hali ya kawaida ya rangi yake baada ya muda mrefu kidogo tangu maradhi halisi yalipokomeshwa. Bila matibabu maradhi haya huchukua muda kupona hivyo dawa ni muhimu ili mwenye maradhi aweze kupona upesi.
Namna ya kuyatambua
Maradhi haya ni rahisi kuyagundua ila kutokana na kufanana kwake na maradhi mengine yenye dalili kama hizi uhakiki wa vimelea vinavyosababisha maradhi haya ni muhimu.
Sehemu ya ngozi kutoka kwenye eneo lenye maambukizi huchukuliwa na kupelekwa maabara ambako sehemu hii ya ngozi huwekwa kwenye darubini maalum kwa ajili ya kuangalia vimelea hivi vya fangasi.
Nini matibabu yake?
Maradhi haya huweza kutibika kirahisi, ila mara nyingi hurudia kushambulia ngozi hasa eneo ambalo liliwahi kushambuliwa kabla.
Kutokana na uwezo wake wa kurudia kuambukiza ngozi huwa inashauriwa kwa aliyewahi kupata maradhi haya kurudia kutumia dawa ya kuua vimelea vya fangasi mara kwa mara ili kuondoa uwezekano wowote wa maradhi kurudia kushambulia.
Matibabu ya maradhi haya huhusisha dawa za kupaka zinazoua vimelea hivi vya fangasi
Dawa za kuua vimelea vya fangasi za kunywa pia hutolewa kwa ajili ya kutibu aina hii ya fangasi lakini hushauriwa zitolewe tu kama dawa za kupaka zimeshindwa kuua vimelea hivi vya fangasi.
Maradhi yanayofana nayo:
Kuna magonjwa ambayo hufanana na maradhi haya. Mfano ;
-Pumu ya ngozi
-Vitiligo
Maradhi haya tutayazungumzia kwenye makala zijazo kwenye mtiririko huu.
Matokeo baada ya matibabu
Kama nilivyoandika hapo juu maeneo ya ngozi yaliyobadilika rangi huweza kubaki hivyo hata baada ya vimelea vya fangasi kuondolewa na dawa.
Hii inamaanisha inawezekana kabisa mgonjwa akabaki na mabaka yanayotokana na vimelea hivi vya fangasi muda mrefu hata baada ya kutumia dawa ambayo imefanikiwa kuondoa vimelea hivi vya fangasi. Hali hii mara nyingi huchanganya wagonjwa na kusababisha wagonjwa kudhani kuwa maradhi bado upo hivyo kuendelea kutumia dawa au kuanza kutumia dawa baada ya muda mfupi tangu kumaliza kutumia dawa zilizofanikisha uondoaji wa vimelea.
Hali ya sehemu ya ngozi iliyoathiriwa na vimelea vya fangasi kurudisha rangi ya kawaida ya ngozi kama sehemu nyingine ambazo hazikua na madhara huchukua muda mrefu kidogo ingawa kama eneo husika lilikua na uvimbe basi uvimbe hupotea haraka.
IMETOKA KWA:
DR ISAAC MARO

Wednesday, 19 March 2014
Jinsi ya kumsaidia mgonjwa wa kifafa
RAFIKI yako anaanguka chini na kupoteza fahamu. Mwili wake unakakamaa, kisha unaanza kusukasuka. Ukijua kwamba mtu huyo ana kifafa, huenda ukampa huduma ya kwanza. Hebu tuone mambo kadhaa ya msingi kuhusu ugonjwa huu ambao mara nyingi haueleweki.
Kifafa ni nini? Kifafa ni ugonjwa
wa ubongo unaomfanya mtu azimie. Huenda mtu akazimia kwa dakika tano
hivi. Kisa kama kile kilichotajwa katika fungu linalotangulia
kinaonyesha aina ya kifafa inayoitwa kifafa kikuu.
Ni nini humfanya mtu azimie? Watafiti
wanasema kwamba mtu huzimia kunapokuwa na utendaji usio wa kawaida
katika chembe za ubongo. Haieleweki ni kwa nini utendaji huo hutukia.
Ninapaswa kufanya nini nikimwona mtu akipatwa na kifafa kikuu? Tovuti ya Kenya inayoitwa The Beehive inaorodhesha
mambo unayopaswa kufanya: ‘Usijaribu kumzuia kwa kutumia nguvu. Kufanya
hivyo kunaweza kusababisha majeraha kwa mgonjwa na pia kwa yule
anayejaribu kumsaidia. Kusukasuka kunapoanza kupungua, hakikisha ya
kwamba kupumua kumerudia hali yake ya kawaida.’ Tovuti hiyo pia inasema:
“Ikiwa kuzirai kumekaa zaidi ya dakika 5, mpeleke mgonjwa hospitalini.
Hili huwa nadra lakini lifanyikapo huwa hatari sana na ni lazima
umkimbize mgonjwa hospitalini hata ikiwa bado yuko katika hali hiyo ili
kuokoa maisha yake.” Inasema pia unapaswa kumpeleka hospitalini “ikiwa
kuzirai kutaisha na kujirudia tena mara hiyo hiyo kabla ya mgonjwa
kupata nafuu.”
Ninaweza kumsaidiaje mgonjwa anapozimia? Weka
kitu laini kati ya kichwa chake na sakafu, na uondoe vitu vyote vyenye
ncha kali vilivyo karibu na kichwa chake. Mwili wake unapoacha
kusukasuka, mgeuze alalie ubavu wake kama picha kwenye ukurasa unaofuata
inavyoonyesha.
Nifanye nini mgonjwa anapopata fahamu? Kwanza,
mhakikishie kwamba yuko salama. Kisha msaidie asimame wima na umwongoze
hadi mahali anapoweza kupumzika kabisa. Watu wengi huwa
wamechanganyikiwa na wanahisi usingizi baada ya kuzimia; wengine hupona
upesi na wanaweza kuendelea kufanya kazi waliyokuwa wakifanya kabla ya
tukio hilo.
Je, watu wote wanaoshikwa na kifafa husukasuka? La.
Wagonjwa fulani hupoteza fahamu kwa muda mfupi sana bila hata kuanguka
chini. Aina hiyo ya kifafa inaitwa kifafa kidogo, na mgonjwa haathiriki kwa muda mrefu. Watu fulani wanaoshikwa na aina hiyo ya kifafa wanaweza kupoteza fahamu kwa muda wa dakika kadhaa. Hilo
linapotokea, mgonjwa anaweza kutembea huku na huku ndani ya chumba,
avute kwa nguvu mavazi yake, au atende kwa njia ya isiyo ya kawaida.
Baada ya tukio hilo, huenda akahisi kizunguzungu.
Watu wenye kifafa huhisije? Watu
wengi walio na kifafa huwa na hofu kila wakati kwa kuwa hawajui ugonjwa
huo utawashika tena lini na utawashikia wapi. Ili kuepuka aibu, huenda
wakaepuka kuwa mahali palipo na watu.
Ninaweza kumsaidiaje mtu aliye na kifafa? Mtie
moyo aeleze hisia zake. Sikiliza kwa makini. Mwulize angependa
umsaidiaje anaposhikwa na kifafa. Kwa kuwa watu wengi walio na ugonjwa
huo hawaendeshi gari, huenda ukajitolea kumbeba kwenye gari lako au
unaweza kumsaidia kununua vitu na kumfanyia shughuli mbalimbali.
Je, mtu anaweza kupunguza au kuzuia mara anazozimia? Hali
fulani huchangia kuzimia, kama vile kuwa na mkazo au kukosa usingizi.
Kwa sababu hiyo, wataalamu wanawatia moyo watu walio na ugonjwa huo
wapumzike vya kutosha na wafanye mazoezi kwa ukawaida ili wapunguze
mkazo. Katika visa fulani, dawa zimewasaidia wagonjwa wasizimie.
Subscribe to:
Posts (Atom)