Ni kweli washauri wa masuala ya mapenzi wanaeleza kuwa, ili uweze kumshika
vilivyo mpenzi wako unatakiwa kuhakikisha unampa katika kila anachokitaka
lakini hawakuzungumzia ishu ya wewe kukubali mapenzi kinyume na maumbile.
Hawakurusu hilo kwa kuwa wanajua madhara ya kufanya hivyo. Sasa iweje leo
ukubali kufanya dhambi hiyo eti kwa kuwa mpenzi wako kataka na unampenda?
Katika ulimwengu wa sasa wapo wanaume wa ajabu sana. Hawa ni wale ambao si
wastaarabu. Wao hawaangalii madhara yanayoweza kuwapata wenzao bali wanaangalia
kujifurahisha wao tu. Mbaya zaidi baadhi ya wanawake nao wamekuwa mbumbumbu.
Eti kwa kuogopa kuachwa au kusalitiwa wanasema bora wafanye hivyo. Jamani,
ifike wakati tufikirie kila tunalolifanya katika maisha yetu ya kila siku. Zipo
mbinu nyingi za kumridhisha mpenzi wako na wala asifikirie kukuacha wala kukusaliti
bila hata kumkubalia afanye hivyo.
Pia unatakiwa kufahamu kwamba, unaweza kumpa mpenzi/mume wako mapenzi hayo
lakini bado akakusaliti tu. Sasa kwa nini ujidhalilishe?
Ni kamchezo ka’ nyumba ndogo
Ukijaribu kuchunguza utabaini kuwa wanaoongoza kwa mchezo huo mchafu ni wale
wezi wa mapenzi ambao hufahamika kwa jina la nyumba ndogo.
Hawa eti wanatumia mbinu hiyo kuwashika waume za watu. Kimsingi hii ni aibu na
wanaokubali kufanyiwa hivyo wanajidhalilisha na hawawezi kudumu na wanaume wao.
Usithubutu kabisa
Mapenzi kinyume na maumbile licha ya kwamba yamekatazwa hata na vitabu
vitakatifu, madhara yake kiafya pia ni makubwa. Wapo wengi ambao sasa wanajuta
kwa kufanya mchezo huo kutokana na kupata matatizo wakati wa kujifungua lakini
pia wengi wao imekuwa ni rahisi kuambukizwa magonjwa mbalimbali ya zinaa
ukiwemo Ukimwi.
Ni laana
Wanaofanya hivyo wamelaaniwa na wanaweza kushangaa uhusiano wao unakumbwa na
matatizo kisha kusambaratika kwani Mungu hawezi kuubariki ule unaokwenda
kinyume na maagizo yake.
Ni suala tu la kukaa na kujiuliza, wewe mwanamke unapata raha gani kufanya
mapenzi kwa njia ambayo haijaruhusiwa? Wakati mwingine nashindwa hata kuwaelewa
hawa wanaofikia hatua ya kujisifia kuwa eti wanawaachia waume zao ‘wajisevie’
wanachotaka kwa kuwa wanawapenda.
Hivi watakuwa na akili timamu? Kumpenda mtu ndiyo uwe tayari kuhatarisha maisha
yako kiasi hicho? Tena kwa taarifa yako wale wanaowakubalia wapenzi wao mapenzi
kunyume na maumbile wanaonekana wajinga na wanadharaulika. Hakuna mwanaume
anayeweza kumheshimu mwanamke anayeweza kuuweka rehani mwili wake kwa njia
hiyo.
.
Madhara yake kiafya
Hudhoofisha kinga ya mwili na kusababisha maambukizi ya magonjwa ya zinaa na ukimwi
Ifahamike kwamba njia ya haja kubwa ni laini na dhaifu hivyo huweza kuchanika pale inapotumika kinyume na kazi yake na kusababisha matatizo ya prolapse na majipu.
Pia huweza kusababisha maambukizi ya human papilloma virus (HPV) ambayo uchangia saratani katika sehemu za haja kubwa.
Kuharibika na kudhoofika kwa mishipa na misuli katika sehemu ya haja kubwa husababisha matatizo makubwa kipindi cha kujifungua.
No comments:
Post a Comment