Saratani ya matiti ni ya pili kwa ukubwa na mara nyingi
huwapata zaidi wanawake hasa wenye umri zaidi ya miaka 50. Kama unahisi uvimbe wowote au mabadiliko
yoyote yasiyo ya kawaida katika maziwa unatakiwa kuwahi mapema hospitali kwa
uchunguzi kabla tatzo halijawa sugu. Saratani hii hutibiwa mapema katika hatua
za awali kabla haijasambaa katika maeneo mengine ya mwili kupitia mirija, tezi
na mishipa ya damu. Ikumbukwe kuwa
wanawake huweza kuhisi uvimbe, maumivu na maziwa kujaa na kuwa makubwa hasa
kipindi cha hedhi na ujauzito hivyo ni
muhimu kutofautisha hali hii ambayo ni ya kawaida na saratani ya maziwa.
MADARAJA YA SARATANI HII
Kuna aina tatu za madaraja ya saratani ambayo ni:-
DARAJA LA KWANZA ni saratani ambayo husambaa taratibu na
isiyokuwa na madhara
DARAJA LA PILI ni saratani ambayo hukua na kusambaa kawaida
DARAJA LA TATU ni hukua na kusambaa haraka sana na huwa
hatari sana
NINI HUSABABISHA?
Saratani hii husababisha na kukua na kuongezeka kwa seli,
tezi na misuli ya maziwa bila mpangilio wala udhibiti ambayo huchangiwa na
Kuongezeka umri, hatari huongezeka kila baada ya miaka kumi
Mazingira unayoishi
Tatizo kuwepo katika familia kwa muda mrefu
Kama ulishawahi kupata saratani hii au saratani yoyote
Kutomnyonyesha mtoto kwa muda mrefu
Maziwa kuachwa wazi
Kupiga X Ray mara kwa mara
Unywaji wa pombe kupita kiasi
Kutumia dawa za kuzuia mimba kwa muda mrefu
DALILI
Kuwepo kwa madonge na uvimbe katika maziwa bila maumivu
Kubadilika kwa ukubwa na umbo la maziwa
Kusinya katika baadhi ya ngozi za maziwa
Chuchu za maziwa kubadilika na mara nyingi kutoa damu
Mara chache huambatana na vidonda vidogo vidogo katika
chuchu
VIPIMO
Vipimo ambavyo huweza kutumika kutambua kama una saratani ya
maziwa ni pamoja na:-
Uchunguzi unaofanywa na dakitari
Kujichunguza mwenyewe mbele ya kioo
X Ray ya
matiti(Mammogram)
Ultrasound ya matiti
MRI scan ya matiti hasa kwa wasichana wadogo
Biopsy ambapo hutolewa tissue kwa ajili ya uchunguzi
MATIBABU
Matibabu ya ugonjwa huu uhusisha mionzi, dawa hormoni na
upasuaji kutokana na hatua na dalili za ugonjwa chini ya maelekezo ya
wataalamu.
KWA MSAADA ZAIDI BONYEZA
HAPA. TAZAMA VIDEO CHINI KUJUA JINSI YA KUJICHUNGUZA MWENYEWE.
No comments:
Post a Comment