Saturday 29 March 2014

SABABU ZA KUTOKA HARUFU MBAYA UKENI NA NAMNA YA KUJIKINGA



Wanawake na watu wengi huzani kuwa harufu mbaya itokayo ukeni ni matokeo ya uchavu na kutojisafisha vizuri… Matokeo yake huongeza jitihada katika kujisafisha bila mafanikio ya kuondokana na tatizo hili… Kihalisi, badala kusuluhisha, unapojisafisha zaidi ni unaongeza tatizo badala ya kutatua… Japokuwa ni kweli mara nyingine inaweza ikawa ni sababu ya uchafu… Ila mimi naamini walio wengi huwa wanazingatia usafi… Ndo maana nimeona leo tupeane mawazo juu ya tatizo hili, na kujua namna ya kujikinga
VSABABISHI
i. Bacteria

Wednesday 26 March 2014

Tahadhari kuhusu ugonjwa wa dengue nchini

Kutoka GAZETI LA MWANANCHI
Dar es Salaam. Wananchi wameaswa kuchukua hadhari juu ya ugonjwa wa dengue ambao dalili zake ziko sawa na zile za malaria. 
Mpaka sasa ugonjwa huo hauna tiba maalumu wala chanjo na njia pekee ya kukabiliana nao ni kutambua dalili zake kama vile homa, kupungukiwa maji au damu, kuumwa kichwa, maumivu ya viungo na uchovu. Mgonjwa anaweza kupoteza maisha endapo atachelewa kupatiwa matibabu.

Monday 24 March 2014

FAIDA YA KULA NDIZI KWA WAGONJWA WA MOYO NA FIGO

Kula ndizi, ni muhimu sana kwa afya zetu kwani husaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo na mishipa ya damu kama myocardial infarction, kiharusi na kudhibiti shinikizo la damu.

soma na hii:>>>>MAGONJWA HATARI YANAYOTIBIWA NA MBEGU ZA MABOGA

Pia ndizi huweza  kuzuia matengenezo ya vidonda vya tumbo na duodenal ulcer pamoja na kuzuia homa na kuzeeka kwa ngozi kutokana na kuwa na vitamini C na E.

Aidha Ndizi inapendekezwa kuwa ni mlo wa kila siku kwa ajili ya watu wanaosumbuliwa na magonjwa wa figo na moyo.

MAGONJWA 10 UNAYOWEZA KUJITIBU KWA KUTUMIA MBEGU ZA MABOGA:

ZIKIWA zimesheheni protini na madini kadhaa kama vile chuma, kopa, maginizia, manganizi na zinki, mbegu za maboga zinakuwa mbegu bora na muhimu kutafuna kila wakati kama wewe ni mpenzi wa kutafuna-tafuna. Imethibitika pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida lukuki kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10:
01 UGONJWA WA MOYO:
Mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini aina ya maginizia (magnesium) ambayo huboresha utendaji kazi wa viungo vya mwili. Huimarisha usukumaji wa damu kwenye moyo, huimarisha ukuaji wa mifupa na meno, huifanya mishipa ya damu kupitisha damu kwa urahisi na hufanya upatikanaji wa haja kubwa kuwa laini.
02 KINGA YA MWILI:
Mbegu za maboga pia zina kiasi kingi cha madini ya Zinki (Zinc). Madini haya yana faida nyingi mwilini, ikiwemo kuimarisha kinga ya mwili, kuboresha ukuaji na uundaji wa chembechembe hai za mwili, kuboresha usingizi, kuboresha ladha mdomoni na harufu, huboresha afya ya macho na ngozi, hurekebisha sukari na huboresha nguvu za kiume pia.
Upungufu wa madini ya ‘Zinc’ mwilini una uhusiano mkubwa sana na matatizo ya kuzaa watoto njiti, kuota chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo darasani kimasomo na matatizo mengine mengi ya kimwili na kiakili.
03 MAFUTA YA OMEGA -3:
Omega-3 ni moja kati ya mafuta muhimu sana mwilini. Jamii ya karanga pamoja na mbegu za maboga ni miongoni mwa mbegu zenye kiasi kingi cha mafuta aina hii. Hivyo ulaji wa mbegu za maboga utakuwezesha kupata kirutubisho hiki muhimu katika mwili wako na kukupa faida za mafuta haya ambazo ni nyingi.
04 KIBOFU CHA MKOJO:
Tangu enzi za mababu zetu, mbegu za maboga zimetumika kuimarisha afya ya wanaume kutokana na kuwa na kiasi kingi sana cha madini aina ya Zinc ambayo ni muhimu sana kwa afya ya kibofu cha mkojo. Mbegu za maboga pamoja na mafuta yake, yote kwa pamoja hutoa kinga kwenye kibofu kupatwa na matatizo ya kiafya, yakiwemo yale ya saratani ya kibofu.
05 KINGA DHIDI YA SARATANI:
Imethibitika kwamba watu ambao hula mlo wenye kiasi kingi cha mbegu za maboga wamegundulika kuwa na hatari ndogo sana ya kupatwa na saratani za tumbo, matiti, mapafu na kibofu.
06 UGONJWA WA KISUKARI:
Utafiti uliofanywa kwa kuwalisha wanyama mbegu za maboga, umeonesha kuwa ulaji wa mbegu za maboga, husaidia kurekebisha kiwango cha ‘Insulin’ mwilini na hivyo kumuepusha mtu kupatwa na ugonjwa wa kisukari.
07 MATATIZO YA UKOMO WA HEDHI:
Mara nyingi kina mama watu wazima ambao wamefikia ukomo wa hedhi, hupatwa na matatizo mbalimbali yanayosababishwa na hali hiyo. Hata hivyo utafiti umeonesha kuwa mbegu za maboga zina uwezo wa kurekebisha hali hiyo na kuondoa kabisa matatizo ya kiafya yatokanayo na ukomo wa hedhi.
08 AFYA YA MOYO NA MAINI:
Mbegu za maboga, ambazo zina kiasi kingi cha mafuta mazuri, kamba lishe na virutubisho vinavyoimarisha kinga ya mwili (antioxidants), zimeonekana kuwa bora pia kwa afya ya moyo na ini, huweza kumpatia mlaji kinga dhidi ya matatizo ya kiafya katika moyo na ini.
09DAWA YA USINGIZI:
Mbegu za maboga zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha ‘homoni’ za usingizi. Ulaji wa mbegu za maboga saa chache kabla ya kupanda kitandani, hasa ukila pamoja na tunda lolote, kunasaidia kupata usingizi mzuri na tulivu.
10 DAWA YA UVIMBE:
Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa mbegu za maboga zina mafuta yenye uwezo wa kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya uvimbe (inflamatory diseases) sawa na dawa aina ya ‘indomethacin’, lakini mbegu hizi hazina madhara kama ilivyo kwa hiyo dawa.
JINSI YA KULA MBEGU ZA MABOGA
Ili kupata faida zake zote, zikiwemo zile za mafuta yake, inashauriwa kula mbegu hizo zikiwa kavu, bila kuzikaanga. Hakikisha pia unapata mbegu zilizohifadhiwa vizuri ambazo hazijaoza wala kuwa na fangasi. Iwapo utapenda kuzikaanga, basi hakikisha unazikaanga kwa muda usiozidi dakika 15, unaweza pia kuongeza chumvi kidogo kupata ladha, lakini za kukaanga zitakuwa hazina mafuta mengi kama zile kavu

Thursday 20 March 2014

Jinsi Asali inavyoweza kukutibu matatizo mbalimbali



ASALI inafahamika kwa muda mrefu
kama chakula muhimu ambacho pia
kinasaidia sana katika kupambana na
magonjwa mbalimbali na matatizo
yatokanayo na uzee.
Kwa mujibu wa tafiti mpya za
wataalamu wa madawa lishe na vifaa
tiba, imedhihirika kwamba, uwezo wa
asali kutibu unaweza kuongezeka
maradufu kama itachanganywa na
mdalasini.

Madhara na Matibabu ya mba mwilini

Hali hii hutokana na uwezo wa fangasi kusimamisha shughuli za uzalishaji wa homoni na kemikali inayoipa ngozi rangi yake. Hii husababisha upungufu wa kemikali na hivyo mabadiliko ya rangi ya ngozi.
Je, ni vipi hushambulia ngozi?
Maeneo yenye mabaka yanayoletwa na fangasi wa aina hii hubadilika rangi yake na kuwa na rangi hafifu au inayoonekana zaidi (kama ni mtu mwenye rangi ya maji ya kunde basi ngozi iliyoathiriwa hubadilika na kuwa nyeupe au nyeusi sana.
Hali hii hutokana na uwezo wa fangasi wa aina hii kusimamisha shughuli za uzalishaji wa homoni na kemikali inayoipa ngozi rangi yake. Hii husababisha upungufu wa kemikali na hivyo mabadiliko ya rangi ya ngozi.
Upungufu huo ya rangi ya ngozi si wa kudumu, bali ngozi hurudi kwenye hali ya kawaida ya rangi yake baada ya muda mrefu kidogo tangu maradhi halisi yalipokomeshwa. Bila matibabu maradhi haya huchukua muda kupona hivyo dawa ni muhimu ili mwenye maradhi aweze kupona upesi.
Namna ya kuyatambua
Maradhi haya ni rahisi  kuyagundua ila kutokana na kufanana kwake na maradhi mengine yenye dalili kama hizi uhakiki wa vimelea vinavyosababisha maradhi haya ni muhimu.
Sehemu ya ngozi kutoka kwenye eneo lenye maambukizi huchukuliwa na kupelekwa maabara ambako sehemu hii ya ngozi huwekwa kwenye darubini maalum kwa ajili ya kuangalia vimelea hivi vya fangasi.
Nini matibabu yake?
Maradhi haya huweza kutibika kirahisi, ila mara nyingi hurudia kushambulia ngozi hasa eneo ambalo liliwahi kushambuliwa kabla.
Kutokana na uwezo wake wa kurudia kuambukiza ngozi huwa inashauriwa kwa aliyewahi kupata maradhi haya kurudia kutumia dawa ya kuua vimelea vya fangasi mara kwa mara ili kuondoa uwezekano wowote wa maradhi kurudia kushambulia.
Matibabu ya maradhi haya huhusisha dawa za kupaka zinazoua vimelea hivi vya fangasi

Dawa za kuua vimelea vya fangasi za kunywa pia hutolewa kwa ajili ya kutibu aina hii ya fangasi lakini hushauriwa zitolewe tu kama dawa za kupaka zimeshindwa kuua vimelea hivi vya fangasi.
Maradhi yanayofana nayo:
Kuna magonjwa ambayo hufanana na maradhi haya. Mfano ;
-Pumu ya ngozi
-Vitiligo
Maradhi haya tutayazungumzia kwenye makala zijazo kwenye mtiririko huu.
Matokeo baada ya matibabu
Kama nilivyoandika hapo juu maeneo ya ngozi yaliyobadilika rangi huweza kubaki hivyo hata baada ya vimelea vya fangasi kuondolewa na dawa.
Hii inamaanisha inawezekana kabisa mgonjwa akabaki na mabaka yanayotokana na vimelea hivi vya fangasi muda mrefu hata baada ya kutumia dawa ambayo imefanikiwa kuondoa vimelea hivi vya fangasi.  Hali hii mara nyingi huchanganya wagonjwa na kusababisha wagonjwa kudhani kuwa maradhi bado upo hivyo kuendelea kutumia dawa au kuanza kutumia dawa baada ya muda mfupi tangu kumaliza kutumia dawa zilizofanikisha uondoaji wa vimelea.
Hali ya sehemu ya ngozi iliyoathiriwa na vimelea vya fangasi kurudisha rangi ya kawaida ya ngozi kama sehemu nyingine ambazo hazikua na madhara huchukua muda mrefu kidogo ingawa kama eneo husika lilikua na uvimbe basi uvimbe hupotea haraka.
IMETOKA KWA:

    DR ISAAC MARO


Wednesday 19 March 2014

Jinsi ya kumsaidia mgonjwa wa kifafa

RAFIKI yako anaanguka chini na kupoteza fahamu. Mwili wake unakakamaa, kisha unaanza kusukasuka. Ukijua kwamba mtu huyo ana kifafa, huenda ukampa huduma ya kwanza. Hebu tuone mambo kadhaa ya msingi kuhusu ugonjwa huu ambao mara nyingi haueleweki.

Kifafa ni nini? Kifafa ni ugonjwa wa ubongo unaomfanya mtu azimie. Huenda mtu akazimia kwa dakika tano hivi. Kisa kama kile kilichotajwa katika fungu linalotangulia kinaonyesha aina ya kifafa inayoitwa kifafa kikuu.
Ni nini humfanya mtu azimie? Watafiti wanasema kwamba mtu huzimia kunapokuwa na utendaji usio wa kawaida katika chembe za ubongo. Haieleweki ni kwa nini utendaji huo hutukia.
Ninapaswa kufanya nini nikimwona mtu akipatwa na kifafa kikuu? Tovuti ya Kenya inayoitwa The Beehive inaorodhesha mambo unayopaswa kufanya: ‘Usijaribu kumzuia kwa kutumia nguvu. Kufanya hivyo kunaweza kusababisha majeraha kwa mgonjwa na pia kwa yule anayejaribu kumsaidia. Kusukasuka kunapoanza kupungua, hakikisha ya kwamba kupumua kumerudia hali yake ya kawaida.’ Tovuti hiyo pia inasema: “Ikiwa kuzirai kumekaa zaidi ya dakika 5, mpeleke mgonjwa hospitalini. Hili huwa nadra lakini lifanyikapo huwa hatari sana na ni lazima umkimbize mgonjwa hospitalini hata ikiwa bado yuko katika hali hiyo ili kuokoa maisha yake.” Inasema pia unapaswa kumpeleka hospitalini “ikiwa kuzirai kutaisha na kujirudia tena mara hiyo hiyo kabla ya mgonjwa kupata nafuu.”
Ninaweza kumsaidiaje mgonjwa anapozimia? Weka kitu laini kati ya kichwa chake na sakafu, na uondoe vitu vyote vyenye ncha kali vilivyo karibu na kichwa chake. Mwili wake unapoacha kusukasuka, mgeuze alalie ubavu wake kama picha kwenye ukurasa unaofuata inavyoonyesha.
Nifanye nini mgonjwa anapopata fahamu? Kwanza, mhakikishie kwamba yuko salama. Kisha msaidie asimame wima na umwongoze hadi mahali anapoweza kupumzika kabisa. Watu wengi huwa wamechanganyikiwa na wanahisi usingizi baada ya kuzimia; wengine hupona upesi na wanaweza kuendelea kufanya kazi waliyokuwa wakifanya kabla ya tukio hilo.
Je, watu wote wanaoshikwa na kifafa husukasuka? La. Wagonjwa fulani hupoteza fahamu kwa muda mfupi sana bila hata kuanguka chini. Aina hiyo ya kifafa inaitwa kifafa kidogo, na mgonjwa haathiriki  kwa muda mrefu. Watu fulani wanaoshikwa na aina hiyo ya kifafa wanaweza kupoteza fahamu kwa muda wa dakika kadhaa. Hilo linapotokea, mgonjwa anaweza kutembea huku na huku ndani ya chumba, avute kwa nguvu mavazi yake, au atende kwa njia ya isiyo ya kawaida. Baada ya tukio hilo, huenda akahisi kizunguzungu.
Watu wenye kifafa huhisije? Watu wengi walio na kifafa huwa na hofu kila wakati kwa kuwa hawajui ugonjwa huo utawashika tena lini na utawashikia wapi. Ili kuepuka aibu, huenda wakaepuka kuwa mahali palipo na watu.
Ninaweza kumsaidiaje mtu aliye na kifafa? Mtie moyo aeleze hisia zake. Sikiliza kwa makini. Mwulize angependa umsaidiaje anaposhikwa na kifafa. Kwa kuwa watu wengi walio na ugonjwa huo hawaendeshi gari, huenda ukajitolea kumbeba kwenye gari lako au unaweza kumsaidia kununua vitu na kumfanyia shughuli mbalimbali.
Je, mtu anaweza kupunguza au kuzuia mara anazozimia? Hali fulani huchangia kuzimia, kama vile kuwa na mkazo au kukosa usingizi. Kwa sababu hiyo, wataalamu wanawatia moyo watu walio na ugonjwa huo wapumzike vya kutosha na wafanye mazoezi kwa ukawaida ili wapunguze mkazo. Katika visa fulani, dawa zimewasaidia wagonjwa wasizimie.

(Je wajua?) Ndani ya dakika 30 mwili wako hutoa joto ambalo huwezaza kuchemsha nusu lita ya maji.

.

Sinema, michezo ya kompyuta na tv ni hatari kwa Afya ya mwanao

Siku hizi  kuangalia sinema na kucheza michezo mbali mabali ya tv na kompyuta imekua kawaida kwa watoto wadogo. Utafti unaonyesha kuwa wengi wao uathirika na kuwa na afya duni na matatizo ya kisaikolojia. 

Dawa za HIV na uwezo wa kuponya Saratani

Dawa ambayo kwa kawaida hutumika kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI imegunduliwa kuwa ina uwezo wa kutibu Saratani ya kizazi vikamilifu baada ya kipindi cha miezi mitatu katika utafiti uliofanywa Hospitali kuu ya Kenyatta nchini Kenya.
Matokeo ya utafiti huo ni hatua kubwa katika vita dhidi ya Saratani.

Tambua athari za mwanamke kuchelewa kuzaa

Wanawake wanaochelewa kuzaa wanakabiliwa na tisho la kupata matatizo ya afya ya uzazi. Huu sio utafititi tu balo maoni ya daktari mmoja mkuu mjini Nairobi Kenya.
Athari za kuchelewa huko ni pamoja na kukumbwa na utasa, tisho la kupata Saratani ya kizazi na matiti pamoja na matatizo wakati wa kujifungua.

Haya ni madhara ya Kutoboa mdomo na Ulimi

Katika zama hizi za utandawazi na muingiliano baina ya tamaduni zetu za asili na tamaduni za kimagharibi, imekuwa ni kawaida kwa vijana wa rika tofauti na jinsia zote kutoga ulimi, mdomo, kitovu ama kivimbe cha nyusi kwa sababu tofauti tofauti sana.
Hivyo basi, ni muhimu sana kufahama ukweli kuhusu faida ama hasara za kutoga ulimi ama mdomo kabla hujatekeleza azma yako ya kutoga viungo hivi vya mwili.

Kukosa usingizi Hupunguza nguvu za kiume:

Mnamo mwaka 2007, watafiti nchini Marekani walifanikiwa kutoa ripoti inayojaribu kuhusisha ukosefu wa usingizi na upungufu wa homoni ya testosterone miongoni mwa wanaume watu wazima.
Kwa kawaida kiwango cha homoni ya testosterone hupungua kadiri mwanaume anavyozidi kuwa mtu mzima, na kwa baadhi ya wanaume, kupungua huku kwa testosterone huweza kusababisha ulegevu wa mwili, kukosa hamu ya ngono na hata kuvunjika mifupa ya mwili.
Watafiti wanasema kuwa, wapo baadhi ya wanaume walio kwenye miaka 80 bado huweza kuwa na kiwango cha juu cha testosterone sawa na kile kinachopatikana kwa wanaume vijana. Hata hivyo sababu kubwa inayofanya kuwepo na utofauti katika viwango vya testosterone miongoni mwa rika hizo mbili bado hazieleweki sawasawa, ingawa watafiti wanasema kuwa ukosefu wa usingizi miongoni mwa watu wazima na wazee unaweza kuwa chanzo kimojawapo cha kuwepo kwa hali hiyo.

Thursday 13 March 2014

Kulala chali ni hatari kwa mama mjamzito

Wanawake wajawazito wanaopenda kulala chali  wapo kwenye hatari  ya kuzaa mtoto mfu(stillbirth),kulingana na wanasayansi.
Katika utafiti  uliofanyika nchini Ghana, wanawake wajawazito ambao walipenda kulala chali wakati wa ujauzito  walikuwa  kwenye hatari mara tano zaidi ya kuzaa watoto wenye uzito mdogo na  kwa wanawake wengine walizaa watoto wafu.
Utafiti huu ulifanyika nchini Ghana kutokana na kuwa kati ya watoto 1000 wanaozaliwa 20 hadi 50 kati yao huwa ni watoto wafu.
Hata hivyo, utafiti mpya uliofanyika nchini New Zealand pia umehusisha kulala chali kwa mwanamke mjamzito na idadi kubwa ya  watoto wafu wanaozaliwa  katika nchi zenye raia wenye kipato kikubwa.

Matunzo ya nywele kwa mwanamke:

WANAWAKE wengi hasa wale wanaopenda urembo, huangaika kutunza nywele zao
ili ziwe katika muonekano mzuri, haijalishi ni fupi ama ndefu.
Lakini kwa bahati mbaya, kuna baadhi yao wana nywele dhaifu, na ni wazi kuwa
nywele hizo huwa hazina muonekano mzuri.
Wengi wao wanadhani kuvaa wigi, ama kusuka nywele bandia kwa muda mrefu ni
suluhisho la tatizo hilo, kitu ambacho si kweli kwani nywele hizo zinatakiwa matunzo tu na
kuweka nywele bandia husababisha kuwa dhaifu zaidi.
Kama una nywele dhaifu, basi usipende kupaka rangi za nywele, kwani
kuna baadhi ni kali na hudhoofisha mara dufu, kinachotakiwa ni kufanya stiming
mara kwa mara inayoendana na nywele zako.

Tiba asili ya Maumivu ya tumbo:

Watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na tumbo lisilo la vidonda wala ugonjwa wowote ila utasikia anakwambia tumbo linanikata, huenda akawa anavurugikwa na tumbo au imetokea linasumbua tu.

Wednesday 12 March 2014

Sababu za wanawake kukosa hamu ya tendo la ndoa

Wanawake  wengi  nchini  na  duniani  kwa  ujumla  wanasumbuliwa  na  tatizo  la kukosa  hamu  ya  kufanya  tendo  la  ndoa  ( LACK  OF  LIBIDO ) pamoja  na  tatizo  la  kutofika  kileleni.  Inasadikiwa  kuwa, katika  kila  wanawake  kumi, angalau  wanne  kati  yao  wanasumbuliwa  na  tatizo  la kukosa  hamu  ya  tendo  la  ndoa  na  kutofika  kileleni  wakati  wa  tendo.

Faida 10 za kula matango na matikiti maji:

  1. Ulaji wa matango  na matikiti maji husaidia kuboresha kiwango cha maji ambayo huitajika mwilini, hii ni kutokana na matango kuwa na kiwango kikubwa cha maji ambayo husaidia kuondoa taka mwili pamoja na sumu mbalimbali ambazo miili yetu huzipata kupitia vyakula, madawa na hata vinywaji.
  2.  Husaidia kupunguza uzito wa mwili. Kutokana na kuwa na asili ya nyuzi nyuzi au, fibres, humfanya mlaji ajisikie kushiba bila ya kuongeza vitu mwilini ambavyo husababisha mtu aongezeke uzito hivyo kuzuia magonjwa mbalimbali

Kama unahisi Maumivu wakati wa tendo la ndoa dawa iko hapa

KUVIMBA kwa kuta za uke kutokana na kushambuliwa na fangasi (candida albicans ) au bakteria. Kuta hizi huanza kuwa na vijitundu vidogo vidogo na kadiri muda unavyokwenda bila kutibiwa vitundu hivi huongezeka ukubwa na kuwa kama vidonda na hatimaye kuta za uke kuanza kumomonyoka na hali hii huondoa kabisa hamu ya kushiriki tendo.
Matatizo ya shingo ya kizazi (cervical incompetence) kutokana na maambukizi ya fangasi maeneo hayo. Kutoka kwa mbegu za kiume muda mfupi au masaa kadhaa baada ya tendo ni dalili kuu ya tatizo hili. Pia mwanaume anapogonga shingo hii ya kizazi mwanamke huwa kama anatoneshwa kidonda. Hali hii ya mbegu kurudi nje husababisha mwanamke kutoshika ujauzito.

Hizi ni sababu za mwanamke kuota ndevu na matibabu yake:

Kutokana na asili katika uumbaji pamoja na ambavyo sisi wanadamu tumezoea kuona, ni kwamba ni jambo la kawaida kwa mwanamme kuota ndevu.
Lakini endapo ndevu zitaonekana zimeota kwa mwanamke, basi kwa baadhi ya watu wataanza kujiuliza ni kwa nini na pengine wakawa na mitazamo tofauti juu ya mwanamke huyu ambaye ameota ndevu. Baadhi watamuona mwanamke huyu kuwa ni mchafu na asiyejipenda na mitazamo mingine mingine ya tofauti.

Tambua kuhusu ugonjwa wa Ngiri (Hernia)

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Saturday 8 March 2014

Jinsi ya kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu (TB)

Kifua kikuu (TB), ugonjwa huu husababishwa na bakteria waitwao Mycobactrium tuberculosis. Bacteria hawa (chembechembe za ugonjwa) hushambulia mapafu ya hewa. Ukikaa karibu na mgonjwa mwenye T.B. waweza kuambukizwa ugonjwa huo kwani akikohowa hutoa vijidudu hivyo vikasambaa hewani.
Kifua kikuu cha mapafu ni ugonjwa unaoambukiza kwa urahisi sana. Walio na hatari zaidi ya kuambukizwa ugonjwa huu ni wale ambao ni dhaifu, wakosefu wa lishe bora na wale wanaoishi na mtu mwenye ugonjwa huo.
Ili kukijinga na kumponyesha mgonjwa aliyekwisha upata ugonjwa huo ni lazima mgonjwa atibiwe mapema. Na hili haliwezekani mpaka dalili zake zifahamike.

Wavutaji wa sigara na hatari ya kupata saratani

Kemikali za sumu zilizoko katika tumbaku na sigara huharibu DNA za mwili wa binadamu dakika chache tu baada ya mtu kuanza kuvuta sigara. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni, kemikali hizo zinazoitwa Polycylic Aromatic Hydrocarbons (PAHs) husababisha DNA ziharibike na kuongeza uwezekano wa mtu kupata saratani. Katika uchunguzi huo watalamu walichukua kemikali hizo katika miili ya wavuta sigara na kuzifanyia uchunguzi, ambapo waligundua kuwa, kemikali za PHA hubadilika haraka mwilini na kuwa sumu ambayo huharibu DNA baada ya kupita dakika 15 hadi 30 tangu kuingia tumbaku katika mwili wa binadamu.

Hizi ni hasara za kuzama chumvini:

Tafiti zimeonyesha kuwa,mdomo wa binadamu ki bacteriologia (bacteriologically) ni mchafu maradufu kuliko sehemu ya uke(vagina).
Ni vema kufahamu kuwa,katika hali ya afya,binadamu wote tunaishi na vimelea(microorganisms) katika sehemu nmbalimbali za miili yetu, wakiwa na lengo la kutulinda, kitaalamu wanaita normal flora hawa wanakuwa hawana madhara katika mwili.Hivyo ni kweli kuwa vagina kama ilivyo mdomo una normal flora.

Thursday 6 March 2014

Fanya yafuatayo huweze kupona vidonda vya tumbo.

Watu wengi wamekuwa wakilalamika kutopona vidonda vya tumbo baada ya kutumia dawa mbalimbali sababu wamekuwa wakipatiwa dawa ambazo hazitibu kabisa tatizo hilo bali kupunguza maumivu.Baada ya kufanya utafiti kwa muda mrefu sasa suluhisho la tatizo hilo limepatikana na hakuna tena sababu ya kuishi na vidonda vya tumbo. Unaweza kupona Vidonda vya tumbo amabvyo hupatikana kwenye utumbo mdogo (duodenal alcer) na vidonda kwenye tumbo(Gastric ulcers) endepo utafuata mashariti ya fuatayo:

Jinsi ya Kutambua na Kuthibiti Ugonjwa wa Presha ya Juu:

Presha ya Juu hutokea endapo itazidi kiasi cha140/90mmlHg na ikiwa haitibiwi huharibu mishipa ya damu katika macho, misuli ya moyo kuwa minene , kusababisha mshutuko wa  moyo (heart attack), mshipa ya damu safi kuwa migumu, figo kushindwa kufanya kazi (kidney failure) na kiharusi (stroke).  Presha kwa mwanamke mjamzito inaweza kusababisha kifafa cha mimba na kufanya hata kiumbe kufa tumboni. Hivyo ni muhimu kuchunguza presha ya wanawake wote wajawazito.

Wednesday 5 March 2014

Tiba mbadala kwa wanaotoa harufu mbaya mdomoni:


Harufu mbaya ya mdomo husababishwa na kutofanya usafi  pamoja na maambukizi sehemu  mbalimbali za mdomoni au kwenye njia ya hewa  Ili huweze kupunguza na kuzuia hali hiyo fanya yafuatayo:
  1. Fanya usafi wa mdomo na kunywa maji mengi mara kwa mara
  2. Kila baada ya chakula weka maji mdomoni na sukutua kwa muda wa sekunde kadhaa ili kuondoa mabaki ya chakula.
  3. Baada ya kula unaweza kutafna  mchanganyiko wa mbegu za  iliki na  karafuu ambazo husaidia kupunguza harufu mbaya mdomoni
  4. Pia unaweza kusuuza mdomo kwa kutumia   mchanganyiko   Mdalasini, iliki na  karafuu kuua vijidudu na vimelea mbalimbali mdomoni na katika njia ya hewa
  5. Pia unaweza kusafisha mdomo kwa Juice ya limao kwani huzuia kukua na kuenea kwa bakteria na fungasi
  6. Kama umefanya yafuatayo na bado tatizo linaendelea muone dakitari kwa matibabu zaidi.

Tuesday 4 March 2014

Huu ni Ugonjwa hatari wa moyo (Acute coronary syndrome)



Ugonjwa hatari wa moyo (ACS) ni seti ya ishara na dalili zinazohusiana na kupungua kwa damu inayoingia kwenye misuli ya moyo na kusababisha anjaina na shambulio la moyo (heart attack)
Baadhi ya dalili za ugonjwa kali wa moyo ni pamoja na anjaina isiyo thabiti na aina mbili ya uinifarakti wa misuli ya moyo ambapo misuli ya moyo huaribika. Aina hizi hupewa majina yake kulingana na matokeo ya mchoro uchunguzimeme wa moyo (ECG / EKG) kama infarkteni ya misuli ya moyo pasipo mwinuko wa miokadia infakti ST(NSTEMI) na infarkteni ya misuli ya moyo iliyo na mwinuko wa sehemu ya ST(STEMI).  Kunaweza kuwa na baadhi ya tofauti kuhusu aina za MI ambazo zaweza kuunganishwa na ugonjwa kali wa moyo.
ACS lazima itofautishwe na anjaina imara, ambayo hutokea wakati wa kujikakamua na huisha wakati wa kupumzika. Kinyume na anjaina imara, anjaina msimamo hutokea ghafla, na mara nyingi wakati wa mapumziko au wakati wa kujikakamua kidogo, ama safu chini ya ujikakamuzi kuliko anjaina iliyotangulia ("crescendo angina"). Anjaina inayotokeza upya pia yaweza kuchukuliwa kama anjaina ya msimamo., kwani inaonyesha tatizo mpya katika mshipa mkuu wa moyo wa koronari.(Coronary Artery)
Hata ingawa ACS ni kawaida kuhusishwa na mvilio wa karonari,inawezakuwa pia kuwa na uhusiano na matumizi ya kokeni. { Ugonjwa wa moyo unaosababisha maumivu ya kifua pia unaweza kutuamwa na safura, bradikadia (moyo kupiga polepole kupita kiasi) au takikadia(moyo kupiga kwa haraka kupita kiasi
Nani yuko katika hatari ya kupata ugonjwa huu
Wagonjwa wa sugari
Kurithi katika familia
Wagonjwa wenye shinikizo la juu la damu
Kuongezeka uzito na mafuta mengi mwilini
Ishara na dalili
Ishara ni pamoja na kupungua kwa damu  kwenye moyo na maumivu ya kifua yanayoshuhudiwa kwa kushikana kwa kifua na huenea kwenye mkono wa kushoto nakwaupande wa pembe ya kushoto ya taya.
Hii inaweza kuhusishwa na kutokwa na jasho (jasho), kichefuchefu na kutapika, na pia upungufu wa kupumua.
Mara nyingi, hisia ni zisizo za kawaida,huku maumivu yakihisiwa kwa njia tofauti ama hata kukosekana kabisa,haswa kwa wagonjwa wa kike na walio na ugonjwa wa kisukari.
 Wengine hupata mapigo ya moyo kwa haraka na yasiyo na mpangilio, wasiwasi au hisia za ghadhabu ambazo karibu ziwakabili na pia hisia ya kuwa na ugonjwa kali.
Maelezo ya usumbufu wa kifua kama shinikizo una matumizi chache ya kusaidia katika kutambua ugonjwa kwani si maalum kwa ACS
Utambuzi wa Ugonjwa
Mchoro uchunguzimeme wa moyo
Katika mazingira ya maumivu kali ya kifua, electrokadiogramu ni uchunguzi ambao mara nyingi hutegemewa katika ubainishaji wa visababu mbalimbali. Iwapo inaonyesha uharibifu kali wa moyo( kuinuka kwenye sehemu ya ST, kuzibwa upya kwa kifungu cha tawi cha kushoto, tiba ya shinikizo la moyo kwa njia ya ukarabatimishipa au kutangua mvilio huashiriwa mara moja.(Angalia hapo chini). Kutokana na kukosekana kwa mabadiliko hayo, haiwezekani kutofautisha mara moja kati ya anjaina isiyo thabiti na NSTEMI.
Upigaji picha na vipimo vya damu
Kwa kuwa ni njia moja ya visababishi vingi vya maumivu ya kifua,mgonjwa huwa na njia tofauti za uchunguzaji kwa idara ya magonjwa ya ghafla, kama vile eksirei, vipimo vya damu(ikijumuishwa pamoja na viweka alama vya misuli ya moyo, kama vile Troponini I ama T, na pia dima ya D iwapo kuziba kwa ateri ya mapafu kunashukiwa na pia utazamaji wa telemeta kwa jinsi moyo unavyopiga.
Kuzuia
Ugonjwa hatari wa moyo mara nyingi huonyesha safu ya uharibifu wa moyo na atherosklerosi. Msingi wa kuzuia atherosklerosi ni kudhibiti sababu ya hatari:kula chakula chenye afya, mazoezi, matibabu ya shinikizo la damu na kisukari, kuepuka sigara na kuthibiti hali za kolesteroli kwenye wagonjwa wa hatari kubwa, aspirin imeonekana kupunguza hatari ya matukio ya moyo na mishipa. Kuzuia kwa pili kumejadiliwa katika miokadia infakti.
Baada ya kupiga marufuku kuvuta sigara katika maeneo yote ya umma iliyoambatanishwa kuletwa katika Scotland Machi 2006, kulikuwa na kupungua kwa asilimia 17 katika kuingiza hospitali kwa wagonjwa wenye hatari za moyo. 67% ya upungufu ilitokea katika wasiovuta sigara.
Tiba
STEMI
Kama ECG inathibitisha mabadiliko inayaopendekeza miokadia infakti (mwinuko wa ST katika viingilio maalum, kifungu-tawi kifungo kipya cha kushoto au ruwaza ya mazoezi ya kweli ya nyuma ya MI), thrombolitiki huweza kupeanwa au ukarabatimishipa wa kimsingi unaweza kufanywa. Kwanza, dawa hudungwa ambayo husisimua kuharibika kwa fibrini,na hapo kuharibu vidonge vya damu vinavyoziba koronari ya moyo Kisha katheta inayopindika hupitishwa kupitia kwa fupa la pacha au ateri ya nusu kipenyo na kuungwa kwa moyo ili kubaini vizuizi katika koronari. Wakati vizuizi kupatikana, vinaweza kushughulikiwa kwa njia ya kimakanika na ukarabatimishipa /0} na kupelekwa stentikama kidonda wanayoita kidonda sugu ndiyo inadhaniwa kusababisha uharibifu wa miokadia. Takwimu zinashawishi kwamba uhamisho wa kugawanya na matibabu ni muhimu  Muda wa kuingiza thrombolitiki ya mlango kwa sindano kulingana na Chuo Cha cha Kadiolojia Cha Marekani(ACC) miongozo yafa kuwa katika dakika 30, ili hali muda wa mlango kwa puto (Njia ya kufanywa au kuwekwa bila kupenya ngozi ya moyo (PCI) unastahili uwe chini ya dakika 90. Ilibainika kuwa kutangua mvilio ina uwezekano wa kufyonzwa ndani ya miongozo ya ACC katika wagonjwa wenye STEMI ikilinganishwa na PCI kulingana na utafiti kudhibiti kesi.
NSTEMI na NSTE ACS-
Kama ECG haionyeshi mabadiliko ya kimfano, neno "non-ST sehemu ya mwinuko ACS" kutumiwa. Mgonjwa anawezakuwa ameteseka kwa "mwinuko wa non-ST MI" (NSTEMI). Usimamizi uliokubalika wa anjaina isiyo thabiti na ugonjwa hatari wa moyo ni matibabu ya ujarabati na aspirin, heparini (kawaida huwa ile ya molekiuli yenye uzito wa chinikama vile enoxaparin) na clopidogrel, na glisereli trinitrati ingine yenye afyuni kama maumivu yataendelea.
Uchunguzi wa damu kwa ujumla hufanywa kwa troponini ya moyo masaa kumi na mbili baada ya mwanzo wa maumivu. Kama hii ni nzuri, uchunguzimishipa wa moyo hufanywa kwa dharura kwani hii ni yenye tabiri shambulio la shinikizi la moyo hivi karibuni. Kama troponini ni hasi, zoezi la tredmili au sintigramu thaliamu linaweza kuliziwa.
ACS inayohusiana na kokeni lazima isimamiwe kwa njia ya sawa na wagonjwa wengine wenye ugonjwa hatari wa moyo ila tu vizuizi vya beta havipaswi kutumiwa na benzodiazepini ipeanwe mapema.

Kucheka mara kwa mara ni tiba ya magonjwa mengi kwa Binadamu

Kama wengi wetu tujuavyo, kiwango cha miaka ya kuishi hasa katika nchi za ulimwengu wa tatu kimepungua sana nyakati hizi, hivyo kila tunaposherekea mwaka mpya tunasherekea pia uzee na utimilifu wa miaka yetu ya kufa, lakini hilo lisitupe hofu kwani wataalam wamegundua maajabu yapatikanayo kwa mtu kucheka.

TUNDA LA STAFELI LINA UWEZO WA KUTIBU MAGONJWA HATARI:

Tunda la stafeli kuwa na uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa hatari, ukiwemo ugonjwa wa saratani. Hata hivyo, utafiti wa kwanza kuonesha uwezo wa stafeli kutibu saratani, uligundulika tangu miaka ya sabini, lakini ulifanywa siri hadi hivi karibuni ulipowekwa bayana tena.

Namna ya kujichunguza kama una saratani ya matiti:

    
Saratani ya maziwa ni moja ya magonjwa yanayoongoza katika kusababisha vifo kwa kina mama duniani. Lakini licha ya ugonjwa huo kuwa tishio iwapo tutajizoeza kujipima sisi wenyewe mara kwa mara ili kuangalia iwapo tuna dalili za ugonjwa huo, suala hilo linaweza kusaidia kutambua uwepo wa ugonjwa huo mapema na kuanza matibabu haraka, na hivyo kuepusha vifo vya mamilioni ya wanawake duniani kila mwaka. Kutokana na idadi kubwa ya vifo na kesi za kansa ya matiti duniani, wataalamu wanatuambia kuwa, utambuzi wa awali husaidia kupunguza vifo na mateso yanayotokana na ugonjwa huo kwa kiasi kikubwa. Pia utambuzi wa mapema wa ugonjwa huo hupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa na hata serikali huika. Kwa mfano nchini Tanzania , rekodi za hospitalini zinaonesha kuwa, kila mwaka wanawake 2,500 wa nchi hiyo wanaripotiwa katika hospitali kuu wakisumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya matiti.  Kati ya hao 2,500, wanawake 300 tuu ndo wanaoweza kuendelea na matibabu ya mionzi au upasuaji wa ugonjwa huu kupitia wataalamu wa ugonjwa huo nchini humo. Lakini wanaobakia ambao ni wengi huwa hawawezi kuendelea na tiba kutokana na kushindwa kugharamia tiba ya ugonjwa huo na sababu nyinginezo. Mara nyingi na kwa bahati mbaya  wagonjwa wengi mara wanapogundua kwamba wana kansa ya matiti huwa tayari ugonjwa huo hatari umeshasambaa katika mwili na mishipa ya limfu  na hivyo wataalamu wa tiba huwa na muda mchache wa kumsaidia mgonjwa, na mara  nyingine pia baada ya kipindi kifupi  mgonjwa huwa katika steji za mwisho za ugonjwa huo. Yote hayo yanaonesha umuhimu wa kila mwanamke kufahamu namna ya kujichunguza ili kufahamu kama ana ugonjwa huo au la.

Monday 3 March 2014

Dawa za kiungulia zinasababisha mpasuko wa mifupa:

Maafisa wa afya wanatahadharisha juu ya utumiaji wa muda mrefu wa dozi kubwa ya dawa za kuondoa kiungulia, (heartburn) na kusisitiza kwamba zinasababisha mifupa kupasuka. Dawa hizo ni zile zinazojulakana kama Proton Pumping Inhibitors (PPI) zinazozuia kiungulia na ambazo hutumiwa kudhibiti kiwango cha asidi katika tumbo na pia kutibu ugonjwa wa GERD au gastroesophageal reflux disease. Taarifa hizo zilizotolewa na Kitengo cha Kusimamia Vyakula na Dawa cha Marekani (FDA) zinasema kwamba, dawa hizo za kingulia huongeza uwezekano wa kupasuka mifupa ya nyonga (hip), mikono na ute wa mgongo kwa watu wazima, hasa iwapo dawa hizo zitatumiwa kwa mwaka mmoja au zaidi, au kwa dozi kubwa.

Sababu za kukoroma na jinsi ya kuzuia hali hiyo:

Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala ambalo linaweza kuwatokea watu wa kila umri ingawa hutokea mara nyingi kwa wanaume au watu wanene. Kukoroma huzidi kwa kadri umri unavyoongezeka na asilimia 54 ya watu wazima hukoroma baadhi ya wakati huku asilimia 25 ya wengine wakiwa na tabia ya kukoroma kila wakati. Kukoroma baadhi ya wakati kwa kawaida sio tatizo kubwa na mara nyingi huleta tu karaha kwa mtu anayelala karibu na mkoromaji. Hata hivyo kukoroma huko sio tu kwamba huharibu usingizi wa anayekoroma bali pia huwasumbua na kuwakeresha wanaolala karibu na mkoromaji. Wale wenye tabia ya kukoroma, hukoroma kila wanapolala na mara nyingi huchoka wanapoamka, na watu wa aina hii hushauriwa kumuona daktari na kushauriwa kuhusiana na tatizo hilo. Lakini kabla hatujaendela mbele ni bora tujue kukoroma hasa ni nini au hutokea vipi?

.