Saturday, 9 August 2014

TATIZO LA UKE KUWA MKAVU NA MATIBABU YAKE

Tatizo la kuwa na uke mkavu hutokana na kupungua kwa hormoni aina ya estrojeni katika mwili wa mwanamke ambayo husababisha kudhoofika na kusinyaa kwa misuli ya uke kukosa vilanisho. Hii utokea mara nyingi kwa wanawake wasioskia hamu ya tendo la ndoa, waliojifungua, wanaonyonyesha, wazee na ambao wako katika hedhi. Hii huweza kusababisha maumivu makali kipindi cha tendo na kukuweka katika hatari ya kupata maambukizi ya zinaa na UTI

MATIBABU YAKE.

Matibabu ya tatizo ili mara nyingi huwa ni cream. mafuta au vidonge vyenye vichocheo vya estrojeni iliyopungua katika mfumo wa uzazi kama Estrace, Premarin, Estring na Vagifem kwa maelekezo ya dakitari na kama tatizo linaambatana na dalili nyingine hatari sindano huweza kutumika.
TIBA MBADALA
Tumia vilainisha asili, asa vilivyotengenezwa kwa kiwango kikubwa cha maji epuka kulainisha kwa kutumia mafuta ya kupaka, sabuni za kuogea na  pafyumu kulainisha sehemu hii.
Pia unaweza kufanya maadalizi ya kutosha kabla ya tendo pamoja na kuweka mawazo yote katika tendo kwa muda huo.

1 comment:

.