Tuesday, 26 August 2014

DAKTARI AFARIKI KWA EBOLA

Daktari wa Ebola ameaga dunia licha ya kupewa dawa ya Zmapp
Daktari mmoja kutoka Liberia ambaye aliambukizwa ugonjwa wa Ebola na kutibiwa na dawa ya ZMAPP ameaga dunia.
Waziri mmoja wa Liberia alisema kuwa dakta Abraham Borbor aliyekuwa miongoni mwa madaktari 3 waliopewa dawa hiyo ambayo haijafanyiwa majaribio aliaga dunia mapema leo .
Kufikia sasa zaidi ya watu 1,400 wameaga dunia kutokana na homa hiyo ya Ebola katika ukanda wa Afrika Magharibi katika mataifa ya - Guinea, Liberia, Nigeria na Sierra Leone.hirika la Afya Duniani, WHO limesema kasi na kiwango cha milipuko hiyo hakijawahi kutokea hapo kabla.
Watu wanaokadiriwa kufikia 2,615 Afrika Magharibi wameambukizwa ugonjwa wa Ebola tangu uzuke mwezi Machi mwaka huu.
SOMA ZAIDI http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/08/140825_ebola_liberia_doctor_zmapp.shtml

No comments:

Post a Comment

.