Baadhi ya tabia zetu ambazo wengi huzifanya pasipo kuyajua
madhara yake na kujikuta zikituharibia ama kuua ubongo au maini ambazo
ni sehemu muhimu mwilini mwetu.
Miongoni mwa tabia zinazoweza kuharibu ubongo wako
1.Kutopata kifungua kinywa
Watu wenye tabia ya kutopata kifungua kinywa asubuhi wana hatari ya
kushusha kiwango chao cha sukari katika damu na hivyo kusababisha
virutubisho viendavyo kwenye ubongo kupungua, hali hii husababisha
ushindwe kufanya kazi.
2.Hasira na hamaki za muda mwingi
Watu wenye tabia hii husababisha pia mishipa ya ubongo kuzidiwa nguvu na
hivyo kupunguza uwezo wao wa akili kufanya kazi ipasavyo.
3.Uvutaji wa sigara na vitu vingine vya moshi
Tabia hizi husababisha sehemu nyingi za ubongo kugandamana na hivyo kudumaa na kusababisha ugonjwa unaoitwa ‘Alzheimer’.
Kumbuka pia chembe za sumu ya moshi ziendazo kwenye ubongo baada ya
kupita mapafuni huharibu mishipa midogo ya kumbukumbu na hivyo kumfanya
mtumiaji awe na uwezo mdogo wa kukumbuka vitu na wakati mwingine
kumbukumbu zake kufa kabisa.
4. Matumizi makubwa ya sukari
Matumizi makubwa ya vitu vya sukari huharibu mchakato wa protini ya
mwili na virutubisho vingine kusambaa vema mwilini na hivyo kusababisha
ukosefu mkubwa wa virutubisho vinavyokuza na kuuwezesha ubongo kufanya
kazi.
5. Mazingira ya hewa iliyochafuliwa
Hii huhusisha mazingira machafu tuishiyo ambayo huathiri hewa
tunayovuta. Uchafu huu wa hali ya hewa kupunguza kwa kiasi kikubwa
kiwango cha hewa ya oksijeni katika hewa. Tukumbuke kuwa ubongo ndiyo
mtumiaji mkubwa wa oksijeni, sasa tunapovuta hewa iliyochafuka
tunapunguza kiwango cha hewa ya oksijeni iendayo kwenye ubongo na hivyo
ukosefu wa hewa hii muhimu katika ubongo huathiri ufanyaji kazi wa
ubongo wa mtu.
6. Tabia ya kukosa kulala vya kutosha
Usingizi huruhusu ubongo wetu kupumzika na hivyo kujirutubisha na
kujipanga vyema. Kukosa usingizi kukizidi huuwa seli za kweye ubongo kwa
kiasi kikubwa.
7.Tabia ya kulala tukiwa tumejifunika vichwa
Najua wengi wetu wakilala hupenda kujifunika gubigubi. Wengine ni mazoea
tu na wengine ni kwa ajili ya hofu. Tunapolala vichwa vyetu vimefunikwa
tunaongeza msongamano wa hewa chafu ya kabon dayoksaidi na kupunguza
msongamano wa hewa safi ya oksijeni katika mazingira ya kichwa. Hewa hii
chafu inapozidi maeneo ya kichwani huuwa uwezo wa ubongo.
8. Tabia ya kuufanyisha kazi na kuuchosha ubongo wakati tunaumwa
Wako watu wenyetabia ya kujilazimisha kuwaza au kufanya kazi wakati
wanaumwa, watu hawa hawataki kupumzika hata kama mwili umekataa. Kufanya
kazi sana au kusoma wakati unaumwa husababisha kupungua kwa ufanisi wa
ubongo na hivyo kuharibu au kuua nguvu ya ubongo.
9. Kukosa mawazo yenye hamasa
Siyo vizuri kukaa tu bila kuwaza vitu vyenye maana, au kuzubaa kizembe
zembe tu. Kufikiri ni njia nzuri sana ya kuuweka ubongo wetu kwenye
mazoezi. Kwa kukosa kuuamsha ubongo wako kupitia kuwaza au kufikiri basi
unasababisha ubongo kunyong’onyea na kuganda.
10.Tabia ya kuzungumza kupita kiasi
Wako watu ambao huongea kama vyerehani, wao hujifanya kila kitu
wanakijua, kila sehemu wamekwenda, kila mtu wanamfahamu hamna hadithi
wasiyoweza kuiongelea.
No comments:
Post a Comment