Thursday 31 July 2014

TAHADHARI: VIJIDUDU HATARI VYA MALARIA VYAGUNDULIKA.

Watafiti wametoa tahadhari kuwa vijidudu vya malaria visivyoweza kuuawa kwa dawa vimetapakaa katika maeneo ya mpakani kusini mashariki mwa Asia vikitishia mapambano dhidi ya Malaria.
Vipimo kwa wagonjwa 1000 katika maeneo ya Cambodia, Burma, Thailand na Vietnam vimegundua vijidudu hivyo havizuiliwi na artemisinin dawa inayoaminika katika vita dhidi ya malaria. Utafiti huo umeeleza kuwa kuyarudia

VYAKULA VINAVYOONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA


PILIPILI
Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho kutoka au kamasi kutoka. Kwenye pilipili kuna kitu kinaitwa capsaicin ambacho hufanya pilipili iwe na hali ya ukali ambao huwezesha ubongo kutoa homoni ya endorphins ambayo katika hali ya juu huleta mgusu wa hisia za raha. Pia pilipili husisimua mfumo wa ufahamu (nerves) wa ubongo na katika kufanya hivyo huwezesha kumshwa haraka kimapenzi (kunyegeka) na pia ili ukiguswa au kubusiwa au kunyonywa au kupapaswa uweze kupata hisia kila sehemu

Monday 28 July 2014

TAMBUA MAPEMA KAMA UNA TATIZO LA SARATANI YA MATITI



Saratani ya matiti ni ya pili kwa ukubwa na mara nyingi huwapata zaidi wanawake hasa wenye umri zaidi ya miaka 50.  Kama unahisi uvimbe wowote au mabadiliko yoyote yasiyo ya kawaida katika maziwa unatakiwa kuwahi mapema hospitali kwa uchunguzi kabla tatzo halijawa sugu. Saratani hii hutibiwa mapema katika hatua za awali kabla haijasambaa katika maeneo mengine ya mwili kupitia mirija, tezi na mishipa ya damu.  Ikumbukwe kuwa wanawake huweza kuhisi uvimbe, maumivu na maziwa kujaa na kuwa makubwa hasa kipindi cha hedhi na ujauzito  hivyo ni muhimu kutofautisha hali hii ambayo ni ya kawaida na saratani ya maziwa.

MBEGU ZA MABOGA ZINA UWEZO WA KUKUEPUSHA NA MAGONJWA 10 HATARI

 Zikiwa zimesheheni protini na madini kadhaa kama vile chuma, kopa, maginizia, manganizi na zinki, mbegu za maboga zinakuwa mbegu bora na muhimu kutafuna kila wakati kama wewe ni mpenzi wa kutafuna-tafuna. Imethibitika pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida lukuki kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10:

Thursday 17 July 2014

MADHARA YA VIPODOZI NA PAFYUME

Vipodozi ni mojawapo ya vitu ambavyo humfanya mtu avutie na kubadili na kuongeza mwonekano, umbo na harufu ya binadamu. Hii inaweza kujumuisha cream, losheni, poda, pafyuma, body spray, waves, mafuta ya kuogea, deodoranti, kucha na kope za kubandika, lipsticks na lipshine,  shampoo na vipodozi vya aina mbali mbali. Pamoja na kuongeza mvuto wa ngozi na mwili vipodozi huweza kusababisha madhara yafuatayo:
Magonjwa ya ngozi hili ni tatizo sugu kwa watumiaji hasa wa muda mrefu wa vipodozi kwani husababisha kuungua. kuvimba, kuharibika na kutoka vipele kwenye ngozi ambayo huchukua muda mrefu kutibika au kutotibika kabisa.
Muwasho na Allergy hii huweza kuathiri ngozi, maskio, tumbo na mifumo wa upumuji na fahamu kutokana na harufu kali au kemikali zilizopo katika vipodozi hivyo kumpasa mtumiaji kuwa makini na uchaguzi wa vipodozi.

Wednesday 16 July 2014

HABARI NJEMA KATIKA VITA DHIDI YA UKIMWI

Kuna uwezekano kuwa janga la ukimwi huenda likadhibitiwa ifikapo mwaka 2030, kulingana na ripoti iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi.
Ripoti hiyo imesema kuwa idadi ya visa vya maambukizi mapya na vifo kutokana na HIV, vimeendelea kushuka.
Na shirika la misaada la Medecins Sans Frontieres limeonya kuwa watu wanaoishi na virusi hivyo hawapati dawa za kutosha.
Kwa mujibu wa shirika hilo watu milioni 35 wanaishi na virusi vya HIV.
Ripoti hiyo ilionyesha visa vipya vya maambukizi milioni 2.1 vilitokea mwaka 2013. Idadi hii iko chini kwa asilimia 38 ikilinganishwa na mwaka 2001.
Vifo kutokana na HIV pia vimepungua kwa asilimia 5 katika miaka mitatu iliyopita. Kwa sasa watu milioni 1.5 hufariki kutokana na ugonjwa huo kila mwaka.
Afrika Kusini na Ethiopia zimepiga hatua katika kupunguza vifo vya wagonjwa wa HIV

.IMETOKA http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/07/140716_hiv_unaids.shtml

MATOKEO YA UALIMU 2014

BOFYA HAPA KUANGALIA MATOKEO YA UALIMU 2014

MAOKEO KIDATO CHA SITA 2014


 BOFYA HAPA KUANGALIA MATOKEO

Monday 14 July 2014

JE WAJUA?: UYOGA NI KINGA YA MAGONJWA

Uyoga hufanya damu kuwa nyepesi, unazuia saratani, unashusha kiwango cha kolestro, huchangamsha mfumo wa kinga ya mwili na hudhoofisha virusi

Wednesday 9 July 2014

Ugonjwa wa Mtoto Jichoni (Cataracts)

Mtoto jichoni ni nini?
Huku ni kuwa na mawingu kewnye kioo asili cha jicho (natural lens) kioo hiki ndicho hukuwezesha kuelekeza mishale ya nuru ili kutoa sura ilizo dhahiri. Huweza kutokea katika jicho moja au yote na husambaa kutoka jicho moja hadi lingine.
Baadhi ya mambo yanayosababisha mtoto jichoni ni:

TATIZO LA UVIMBE KATIKA KIZAZI KWA WANAWAKE




Tatizo hili la uvimbe ambao sio saratani huwatesa wakina mama na wasichana wengi na hivyo kufikia hatua ya kuondolewa kizazi endapo hautowaiwa na kutibiwa katika dalili za awali.   Ugonjwa huu kwa kitaalamu huitwa fibroids au leimyoma na huathiri zaidi ya asilimia 25 ya wanawake wa kiafrica na asilimia 50 ya wazungu. Uvimbe huu huwa katika umbile la misuli laini na myembamba na hukua siku hadi siku kutokana na vichocheo vya estrogeni hasa kipindi cha hedhi na ujauzito.
 Uvimbe huu hujitokeza katika ukuta wa kati, wa nje, au ndani kabisa ya nyumba ya uzazi na huambatana na dalili zifuatazo.

.