Sunday 27 April 2014

UMUHIMU WA KWENDA HAJA NDOGO KILA BAADA YA TENDO LA NDOA

Mara nyingi tunashauriwa kukojoa kila baada ya tendo la ndoa. Japokuwa wanawake wengi pamoja na kuwa na hamu ya kwenda haja ndogo kila baada ya tendo ila kutokana na uvivu na uchovu ujikuta katika usingizi mzito na kusahau tendo hili muhimu baada ya kufika kileleni. Umuhimu wa tendo hili ni kupunguza na kuzuia uwezekano wa kupata maambukizi ya magonjwa ya njia ya mkojo(U.T.I) na magonjwa ya zinaa(S.T.I)

Ikumbukwe kuwa tendo la ndoa huongeza presha kwenye kibofu na kusababisha hamu ya kukojoa kila baada ya tendo hali inayokuwezesha kuondoa vimelea vya magonjwa mbali mbali  kabla ya kusambaa kwenye kibofu na sehemu nyingine za mwili  kusababisha matatizo makubwa. kwa wanaotumia kondomo pia unashauriwa kufanya hivo endapo itapasuka sambamba  na kusafisha sehemu za uke na uume kwa maji safi na sabuni.
kwa wanaofanya mapenzi ya mdomo(chumvini na kulamba kone) unashauriwa kutoingiza shahawa, maji maji ya uke/ume na damu mdomoni kwani kuna hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa, ukimwi na hepatitis B.
BONYEZA HAPA KWA MSAADA ZAIDI:




No comments:

Post a Comment

.