Mara nyingi tumezoea kuwaona watu wengi wanaotumia kinywaji
cha bia wakiwa na vitambi. Hali hii husababishwa na upungufu wa proteini aina ya Albumin ambayo hutoka nje ya mishipa ya damu
na kuvuta maji maji nje ya mishipa hiyo ambayo hujaa na kujikusanya sehemu za tumbo na miguu .
Hali hii huweza kuambatana na kukosa hamu ya kula, kiungulia
cha mara kwa mara, kushiba mapema, kukoroma na kupumua kwa shida au maumivu ya tumbo na mgongo sambamba na mrundikano wa mafuta katika sehemu za tumbo.
Pia pombe huharibu na kuingilia kazi za ini ivyo kupunguza
hutengenezwaji wa aina hii ya protein pamoja na kuongeza presha katika mishipa
ya damu ya ini(portal vein) ambayo ulazimisha maji kurudi na kujaa tumboni.
Matatibabu yake ni pamoja na kuacha au kupunguza kiasi cha
pombe kwa siku pamoja kutumia dawa za Diuretics kama Lasix na Aldactone ambazo
utolewa hospitali kwa ajili ya kupunguza maji yaliojaa tumboni ambayo baadae huweza
kupelekea kuvimba miguu na kusababisha madhara katika
sehemu nyingine za mwili kama mapafu. Kibovu na moyo hivyo kupelekea magonjwa
mbalimbali.
Pia sindano kubwa hutumika katiaka hospitali za kisasa
kuondoa maji maji yaliojaa tumboni kwa njia ya Paracentesis.
No comments:
Post a Comment