Mwanamke anapokuwa mjamzito huwa na wasi wasi na kushindwa kugundua kama ujauzito aliobeba ni mtoto wa kike au wa kiume. Kuna njia mbalimbali ambazo wakunga, wataalamu wa afya na wanawaake wazoefu huzitumia kutambua jinsia ya mtoto aliyeko tumboni ambapo mara nyingi asilimia zaidi ya 50 huwa ni kweli. Zifuatazo ni dalili na njia zinazotumika kutambua jinsia:-
1. Tumbo, wazoefu wanaamini endapo utakuwa umebeba uzito mdogo tumboni na tumbo dogo mtoto atakuwa ni wa kume.
2. Haja ndogo, endapo mama mjamzito anatoa haja ndogo rangi nyeusi kuna uwezekano mkubwa amebeba mtoto wa kiume huku nyeupe au rangi ya mawimbi ikimaanisha jinsia ya kike.
3. Chunusi, uwepo wa chunusi nyingi na mara kwa mara ni ishara kuwa umebeba mtoto wa kiume wakati ngozi kuwa laini sana kupita awali ikimaanisha ni mimba ya mtoto wa kike.
4. Maziwa, pale ziwa la kulia linapokuwa kubwa kuliko ziwa la kushoto inamaanisha mimba ni mtoto wa kiume.
5. Miguu kuwaka moto na kuwa laini ina maanisha mimba ni ya mtoto wa kike wakati miguu kuwa na mikono kuwa ya baridi ni mtoto wa kiume.
6. Mapigo ya moyo, hii hutumiwa na wataalamu wa afya ambapo mapigo chini ya 140 ni mtoto wa kiume wakati zaidi ya 140 ikimaanisha mtoto wa kike.
Nywele, mwanamke anapokuwa mjamzito na nywele zikaota au kukua kwa kasi inamaanisha mtoto wa kiume wakati kinyume chake ni jinsia ya kike.
7. Kutamani vyakula, mjamzito anapotamani sana vyakula vya uchachu na chumvi nyingi kuna uwezekano wa kujifungua mtoto wa kiume wakati vitamu na sukari nyingi ni mtoto wa kike.
8. Mtindo wa kulalia ubavu wa kushoto mara nyingi ni jinsia ya kiume wakati ubavu wa kulia ni mtoto wa kike.
9. Kutapika, wengine wanaamini kichefuchefu na kutapika sana nyakati za asubuhi ni ishara ya kubeba mtoto wa kike.
10. Nyingine ni kuongezeka uzito kupita kiasi ikimaanisha mtoto wa kike huku kupungua, kubaki na uzito uleule au kuongezeka uzito kiasi ni ishara kuwa ni mtoto wa kiume
.BOFYA HAPA KULIKE PAGE NA TUSHIRIKISHE NJIA ZINAZOTUMIKA KATIKA JAMII YENU KUMTAMBUA MTOTO ALIYEKO TUMBONI.
No comments:
Post a Comment