Mfanyakazi aliyemtibu mgonjwa wa Ebola Thomas Eric Duncan nchini
Marekani kabla hajafariki asemekana kukutwa na virusi vya Ebola kutokana
na utafiti wa afya aliofanyiwa. Mfanyakazi huyo ambaye jina lake
limehifadhiwa amewekwa kwenye kitengo maalum inasemekana kwamba alivaa
mavazi maalum ya kumkinga na ugonjwa huo wa Ebola.
Duncan ambaye alipata virusi hivyo vya Ebola alipokuwa mjini Liberia
alifariki Jumatano. Mlipuko huo vya virusi vya Ebola kutoka miji ya
Liberia,Guinea na Sierra Leone imethibitishwa kuwa na waathirika 8300 na
vifo vya kukaribia 4033.
Hospitali imethibitisha kuwa njia za kujikinga na maambukizi hayo ya
Ebola zinafatwa kwa auangalizi mkubwa na wafanyakazi wote ambao
wanafanya kwenye kituo hicho cha afya cha Texan Health Presbyterian.
Mkuu wa kituo hicho cha afya Dr. Tom Frieden (CDC) alisema kuna
uwezekano mfanyakazi huyo hakufata njia zote husika za kujikinga na
ugonjwa huo.
Mkuu wa kituo hicho cha afya alikiambia chombo cha habari cha
Marekani CBS kwamba watafanya uchunguzi ili kujua ni jinsi gani muhudumu
huyo wa afya alipata virusi hivyo vya Ebola. Alisema wafanyakazi wote
ambao walimuhudumia Duncan watafanyiwa uchunguzi ili kujua kama na wao
wamepata virusi hivyo vya Ebola.
CHANZO: http://millardayo.com/
No comments:
Post a Comment