Madaktari wengi wanashauri kunywa madawa ya vitamin sababu wajawazito
wengi hawali vizuri. Madini ya muhimu kwa mtoto ni kama yafuatayo;
Calcium, Iron, Folate (B vitamin). Haya madini yote yanaweza kupatikana
kwenye vyakula vifuatazo;
Calcium:
Mtoto anahitaji Calcium kwa ajili ya kukuza viungo vya mwili na mifupa
kukomaa vizuri. Mwili wako unanyonya Calcium inayohitajika na mtoto
hivyo basi unahitaji kula vyakula vitakavyoongeza kiasi hichi mwilini.
Lakini pia ili Calcium inyonywe na mwili unahitaji kukaa juani kwa
kipindi kama cha dakika kumi kila siku. Calcium hupatikana kwenye,
maziwa, mboga za majani kwa wingi, Mayai (Hakikisha yameiva vizuri
)Samaki (esp mifupa lakini sio samaki wote wanashauliwa kula wakati wa
mimba), maharage ya soya, na mchele.
Madini ya Chuma (Iron)
Chuma ni muhimu kwa utengenezaji wa damu, kwani kipindi hichi damu
nyingi inahitajika kwa ajili ya kumpelekea mtoto chakula. Wajawazito
wengi huwa vichanga vyao vinakufa sababu ya ukosefu wa damu toka kwa
mama. Iron hupatikana toka kwa vyakula kama; Mboga za majani kwa wingi
zaidi (Matembele yana Iron zaidi, mchicha, brocolli, sukuma wiki n.k).
Chai na Kahawa huwa inasaidia kuzuia kunyonywa ka iron mwilini hivyo
epuka kunya chai nyingi na ikiwezekana uache kunywa kahawa kwa kipindi
hiki.
CHANZO MTOTO NA AFYA
No comments:
Post a Comment