Si
kila mwanamke yuko huru kusema kuwa aliwahi kupata tatizo sehemu za
siri. Karibu nusu ya wanawake wote walishapatwa UTI na wengi
huwarudiarudia kiasi kwamba inakuwa kero. Nikianza na UTI, napenda
tufahamu maana yake kwanza, UTI ni kifupi cha maneno ya kiingereza Urinary Tract
Infection (UTI), wazazi wengi wanaujua sana kwa sababu ya watoto chini
ya miaka mitano husumbuliwa na ugonjwa huu. Maana halisi ya UTI kwa
Kiswahili ni maambukizi katika njia ya mkojo.
Napenda
wanawake wanosumbuliwa na UTI wajue kuwa njia ya mkojo sio njia ya
uzazi. Wapo wanaofikiri kuwa uke una njia moja ya uzazi na mkojo.
Hapana. Njia ya mkojo inaachana na njia ya uzazi mwanzoni tu mwa uke.
Uambukizo katika njia ya mkojo unapatikana kwa njia mbalimbali, tukiacha magonjwa ya kujamiiana, uambukizo
wa njia ya mkojo unasababishwa na bakteria waishio ukeni au kwenye
utumbo wa binadamu. Bakteria waishio ukeni hawana madhara ukeni, lakini
wakihama na kuingia kwenye njia ya mkojo husababisha matatizo.
Hii inaweza
kutokea wakati wa ngono kwani wakati huo msuguano husababisha wale
bakteria kutoka na majimaji na kufika kwenye tundu la mkojo na kuingia
ndani. Wataalamu wanasema kuwa mwanamke anayefanya ngono
mara kwa mara anaweza kuwa na UTI zaidi ya yule asiyefanya. Bakteria pia
wanaweza kuhama kutoka sehemu ya haja kubwa na kuingia kwenye tundu la
mkojo.
Hutokea
wakati wa kujisafisha na hasa kama mabaki ya kinyesi hubakia sehemu ya
haja kubwa. Njia nyingine iwapo mwanamke atakuwa na tabia ya kubana
mkojo kwa mda mrefu, kibofu cha mkojo kina misuli inayosadia
mwanamke asiende kukojoa anapobanwa na mkojo mpaka atakapokuwa tayari.
Iwapo atahisi kukojoa na asiende baada ya muda mrefu, ataichosha misuli
ya kibofu kiasi kwamba hata siku anayokuwa na mkojo akikojoa hautoki
wote na ule mkojo kidogo unaobaki kwenye kibofu huweka bakteria na
kusababisha maambukizo. Dalili za UTI ni kujisikia kwenda haja ndogo
mara kwa mara na utakapoenda unatoka mkojo kidogo tu. Utasikia mkojo
ukichoma
wakati unatoka na mwisho utasikia maumivu makali. Ikiendelea unaweza
kusikia maumivu ya chini ya tumbo na kiuno. Hata hivyo, kuna magonjwa
mengine yenye dalili kama hizo na ni daktari atakayekusaidia
kutofautisha.
Habari njema ni kwamba UTI inatibika kirahisi kwa antibiotiki, lakini
unashauriwa kumuona daktari kabla ya kuzitumia kwani wakati mwingine
kunywa maji mengi kunasaidia kusafisha njia ya mkojo. Unashauriwa
kwenda
haja ndogo mara unapojisikia kufanya hivyo, yaani kutobana mkojo kwa
muda mrefu sana, kuhakikisha unajisafisha vizuri baada ya haja kubwa na
baada ya kufanya ngono
No comments:
Post a Comment