Madaktari na waalamu wa afya wanashauri
kulala bila nguo za ndani wakati wa usiku ili kuwezesha viungo vya uzazi
kupata hewa ya kutosha ili kuepuka maambukizi ya fangasi na kutoa
harufu mbaya katika sehemu za siri. Kuvaa nguo za ndani wakati wa kulala
usababisha kubana sehemu za siri na joto kupita kiasi ambayo usababisha
joto kupita kiasi na unyevu na kuvutia ukuaji wa fangasi na bakteria
kwa jinsia zote huku pia zikisababisha upungufu wa mbegu za kiume na
harufu mbaya.
Tambua kuwa joto la mwili ushuka kiasi
unapolala na kukuwezesha kupata usingizi mzuri wakati wa usiku hivyo
kulala na nguo za ndani au nguo zozote zinazobana ni kinyume chake na
huongeza mikunjo kweneye ngozi na kupunguza uzuri wa ngozi. Ikumbukwe
kuwa hii haiwausishi wanawake au wanaume wenye matatizo maalumu
yanayowapaswa kuvaa nguo za ndani usiku kama hedhi kwa wanawake na
matatizo ya uzazi. Hivyo ni muhimu kulala bila nguo za ndani au nguo
zinazobana mwili wako ili kuepuka madhara haya.
LIKE PAGE NA WASHRIKISHE MARAFIKI.
No comments:
Post a Comment