Wanawake wengi hulalamika kuwa wanaume ni watata kwenye mapenzi.
Hulaumu kwamba ni ngumu kubaini vitu ambavyo wanaume huhitaji kutoka kwa wanawake.
Wanadai
kuwa wakati mwingine hujitahidi kadiri ya uwezo wao kuhakikisha
wanawapa furaha lakini wanaume huwa hawana hata msisimko.
Hapa
chini, nimekuandalia vitu ambavyo wanaume huhitaji kwa wanawake wao.
Moja kwa moja, mambo yakienda chanya huwa ni zaidi ya chombezo na
hupagawa.
MAPENZI (Love)
Siku zote wanaume huangalia mapenzi kwa wenzi wao.
Mara
nyingi wanaume huwa wepesi kuonesha mapenzi kwa wanawake wao lakini
ndani ya nafsi zao, hutegemea mambo mengi kama malipo (return) ya
upendo waliotoa kabla.
Wanapenda, kwa hiyo nao huhitaji kupendwa ili waone mambo yanakwenda sawa.
Wanawake wengi huwa wanaficha hisia za kupenda, hili huwaumiza wenzi wao.
Onesha
mabadiliko, muoneshe jinsi unavyoridhishwa na upendo wake kisha
mtamkie kwamba kwake umefika, halafu thibitisha hilo kwa vitendo.
MVUTO (Attractiveness)
Wanaume
huhitaji wapenzi wao wawe na mvuto. Hii inawezekana isiwe na maana
kwa wanawake kwa kushindwa kutambua mvuto wao, unavyoweza kuwa
kibwagizo murua cha mapenzi.
Vaa vizuri upendeze, hakikisha muda wote unakuwa nadhifu.
Muonekano wako ndiyo utamfanya mwenzi wako ajiamini popote.
Kwa hiyo, kupendeza kwako ni bonge la chombezo kwa mwenzio.
UAMINIFU (Trustful)
Wanaume hupenda wanawake wenye uaminifu wa asilimia 100.
Mwanaume
huhitaji mwanamke ambaye muda wote atakuwepo kwa ajili yake
kimapenzi, kubadilishana mawazo na kumshirikisha katika siri za maisha
yake.
Bahati mbaya wapo wanawake wengi ambao hawana uaminifu hata chembe.
Hilo huwafanya wanaume kukosa imani kwa wapenzi wao.
Jiamini kisha uwe muaminifu.
Mfanye mpenzi wako asikutilie shaka ya aina yoyote kisha uone jinsi maisha yanavyoweza kusonga mbele.
FAMILIA (Family)
Wazo
la kila mwanaume anapopata mwanamke, hufikiria ajenge naye familia
haraka iwezekanavyo. Hivyo basi, huhitaji mwanamke ambaye yupo tayari
kwa hilo.
Kitu ambacho huwakera wengi ni pale wanapokutana na mtu aliye na mawazo ya kurukaruka.
Kama umeshaolewa, muoneshe mumeo jinsi ulivyo fundi wa kuiweka familia pamoja.
Ukifanya hivyo, utakuwa umempatia, kwani hakuna jambo ambalo wanaume huwa hawapendi kama kuona familia inasambaratika.
UKARIMU (Kindness)
Wanaume
huwa na matarajio ya kuwaona wanawake wao wakiwa wapole, waungwana na
wakarimu. Jitazame na ujitengeneze kuwa hivyo ili umvutie mwenzi
wako.
Ukorofi, ubishi na roho mbaya siyo sifa ya kike.
UCHESHI (Funny)
Wanaume
hupenda wanawake wanaojua kucheka. Akiwa naye, wazungumze na wacheke.
Wanaume huwachukia wanawake wanaopenda kununa. Kama una tabia hiyo,
jirekebishe ili umkune mwenzi wako.
U-MWANAMKE (Femaleness)
Kwa kawaida, wanaume hupenda wanawake ambao wanajitambua kuwa wao ni wanawake.
Huwachukia wale wanaojipa sifa ya u-dume au wababe, wanaopenda kutoa amri.
Huhitaji
wanawake wanaotimiza wajibu wao kama wanawake kulingana na jamii
inavyotambua. Hupenda wanawake wanaojali, kujiheshimu na kadhalika.
Wale walevi hukosa sifa ya u-mwanamke ambayo wanaume huihitaji.
LIKE PAGE NA TUTUMIE TATIZO LOLOTE LA KIAFYA TUTAKUSAIDIA KULITATUA
No comments:
Post a Comment