Friday 24 October 2014

HALI NI MBAYA KATIKA HOSIPITALI YA OCEAN ROAD.

Hali ni mbaya katika hospitali ya Ocean Raod Dar es salaam kutokana na uhaba mkubwa wa dawa.
Wagonjwa wengi waliolazwa katika hospitali hiyo kwa nyakati tofauti wamesema wameshuhudia wenzao kadhaa wakipoteza maisha kwa kuwa taasisi hiyo haina dawa za kuwatibu.

Muuguzi ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema kuna mgonjwa alifariki jana kwa kukosa dawa huku ndugu zake wakipewa taarifa za kwenda kutafuta dawa lakini hawakurejea hadi ndugu yao alipopoteza maisha.
Katika baadhi ya maduka bei ya baadhi ya dawa walizoandikiwa wagonjwa bei yake ni kubwa hivyo kushindwa kumudu gharama zake.
Chanzo: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

.