Kabla ya kuanza kuuelezea ugonjwa huu ni vyema kufahamu jinsi gani damu husafirishwa katika mwili wa
damu.
Himoglobini (haemoglobin) ni molekyuli ambayo ni sehemu ya
chembe hai nyekundu zilizoko mwilini.Himoglobini hufanya kazi ya
kuzisaidia chembe hai nyekundu kubeba hewa ya oksijenu kutoka kwenye
mapafu kwenda sehemu nyingine za mwili.
Kwa kawaida binadamu
anapozaliwa huwa na himoglobini ya kawaida ambayo huitwa himoglobini A
(Haemoglobin A) au kwa kifupi HbA na Himoglobini ya kichanga ambayo
huitwa Himoglobini F (HbF).Himoglobini A ambayo hutengeneza takriban
asilimia tisini na saba ya Himoglobini za mtu mzima imeundwa na jozi
mbili za minyororo (chains) za alfa (alpha) na beta (beta).
Chembe
hai nyekundu za damu za kawaida huwa laini,za duara na huweza
kujipenyeza katika mishipa ya damu kirahisi.Pia huweza kuishi kwa
takriban siku mia moja na ishirini (120) kabla chembe hai nyekendu za
damu mpya hazijatengenezwa.
Watu wenye ugonjwa wa sickle cell wao
huwa na chembe hai nyekundu ngumu, zenye umbo la mundu au mwezi mchanga
ambazo hupita kwa shida kwenye mishipa ya damu haswa ile midogo.Aina
hii ya himoglobini huitwa Himoglobini S (HbS).Tofauti na chembe hai
nyekundu za damu za kawaida,zenyewe huishi kwa siku chache zaidi, kwa
kawaida takribani siku kumi na sita (16) tu.
Kwa hiyo ugonjwa wa
sickle cell ni ugonjwa wa kurithi ambapo mwathirika huwa na himoglobini S
ambayo hupelekea chembe hai nyekundu za damu zisizo za kawaida
kushindwa kupita kwenye mishipa ya damu kirahisi.Hali hii hupelekea kuwa
na upungufu wa damu kwenye baadhi ya sehemu mwilini.
Hata hivyo
iwapo chembe hai nyekundu za damu HbA ni zaidi ya HbS huweza kutengeneza
HbAS.Hali hii hujulikana kitaalamu kama Sickle cell isiyo na dalili
(Sickle Cell Trait).Watu wenye aina hii ya sickle cell huwa na afya
nzuri ya kawaida.
Ugonjwa wa sickle cell ni ugonjwa sugu na wa
kudumu.Waathirika waweza kuwa wenye afya njema lakini maisha yao
huandamwa na vipindi vya mashambulizi ya maumivu.Umri wa kuishi hupungua
na baadhi ya tafiti za nyuma zinaonyesha kwamba waweza kuishi kwa
wastani wa miaka arobaini (40) mpaka hamsini (50).Ugonjwa huu ni wa
kawaida kwa watu wenye asili ya kiafrika haswa walioko chini ya Jangwa
la Sahara lakini waweza athiri watu wa mataifa mengine pia.
Jinsi ugonjwa unavyorithiwa
Ugonjwa
wa sickle cell waweza kurithiwa kama ilivyo kwa makundi ya damu, rangi
ya ngozi, rangi ya macho na tabia ua vitu vingione vinavyoweza
kurithiwa.
Kwa mfano kama mzazi mmoja ana himoglobini AS,amabyo
huashiria kuwepo kwa sickle cell bila kuonyesha dalili na mzazi akiwa
mzima, basi wana uwezekano wa kupata watoto wenye sickle cell ambao
hawataonyesha dalili.
Pia kama mzazi mmoja ana sickle cell na
mwingine ana sickle cell bila dalili, kuna uwezekano wa asilimia hamsini
ya kupata mtoto mwenye sickle cell au sickle cell bila dalili katika
kila mimba itakayotungwa.
Na kuna takriban asilimia ishirini na tano ya kupata sickle cell yenye dalili katika kila mimba.
Jinsi Sickle Cell inavyotokea
Ugonjwa
wa sickle cell hutokea kutokana na mabadiliko (mutations) katika
mnyororo wa beta (beta chain) ambapo amaino asidi (amino acid) aina ya
glutameti (glutamate) huitoa amaino asidi ya Valini (Valine) kutoka
kwenye nafasi ya sita ya mnyororo wa beta.
Katika mazingira yenye
kiwango kidogo cha oksijeni, chembe hai nyekundu za damu zenye umbo la
kawaida (mviringo) huharibiwa na kupoteza uwezo wa kutanuka na kusinyaa
(elasticity) zipitapo kwenye mishipa ya damu.Hali hii hupelekea chembe
hai hizo nyekundu za damu kuharibiwa na mfumo wa damu kwenye bandama
(spleen) uitwao kwa kitaalamu reticuloendothelial system.
Pia
hupelekea kuziba kwa mishipa midogo ya damu (infarction) kutokana na
chembe hai nyekundu za damu zenye umbo la mundu.Hali hii yaweza
kupelekea kukosekana kwa damu na oksijeni ya kutosha katika baadhi ya
viungo.
Dalili za sickle cell
Ni mara chache kwa dallili
za sickle cell kuonekana katika miezi sita ya mwanzo baada ya
kuzaliwa.Hii inatokana na kuwepo kwa wingi kwa himoglobini ya kichanga,
himoglobini F, ambayo huzilinda chembe hai nyekundu za damu zisibadilike
umbo.
Ikumbukwe kwambamabadiliko ya kiumbo ya chembe hai nyekundu za damu ndiyo chanzo cha dalili tutakazoziona hivi punde.
Dalili utotoni
-Maumivu ya pingili (dactylitis) za mikono na miguu
-Kushambuliwa na maradhi kama uti wa mgongo,
nimonia,mafua,kikohozi n.k
-Kuvimba kwa bandam (splenomegally) kutokana na kujaa ghafla
kwa damukwenye bandama
-Kusinyaa kwa bandama(autosplenectomy)
Dalili ukubwani
-Upungufu wa damu
-Maumivu ya tumbo
-Maumivu ya mifupa (viungo)
-Kupooza
-Maumivu ya kifua yafananayo na nimonia (acute chest syndrome)
-Kubana kwa kifua
-Kukojoa damu
-Vidonda sugu miguuni
-Kusimaama kwa uume kuambatanako na maumivu makali (priapism)
-Kuvimba kwa paji la uso au fuvu
Vipimo na Uchunguzi
Vipimo vifuatavyo ni muhimu katika kugundua sickle cell na magonjwa yaambatanayo na sickle cell
-Kipimo cha Sickling (Sickling Test)
-Kipimo cha damu kama kuna Malaria
-Kipimo cha mkojo kuchunguza uwepo wa chembe hai nyekendu za damu katika mkojo
-Picha ya kifua (x-ray) kuangalia iwapo kuna athari katika kifua
-Kipimo cha wingi wa damu (Hb level)
-Kipimo cha kundi la damu (Blood grouping and cross matching)
Matibabu
Aina
ya matibabu anayohitaji mgonjwa hutegemeana na aina ya mgonjwa na
tatizo linalomsumbua kwa wakati huo. Ni vyema kuchukua hatua mapema
iwapo una mtoto mwenye dalili zilizotajwa hapo juu.
Ushauri
Ugonjwa
wa Sickle cell ni ugonjwa sugu na wa kudumu.Watu wenye ugonjwa huu
huambukizwa kirahisi magonjwa mengine kama vile nimonia, malaria n.k
Wagonjwa wenyewe wanatakiwa kujilinda dhidi ya baridi, magonjwa ya kuambukiza kama nimonia, malaria, magonjwa ya mifupa n.k
Pia
ni vizuri kwa mgonjwa wa nimonia kuoa au kuolewa na mwenza ambaye hana
sickle cell ili kupunguza uwezekano wa kupata mtoto mwenye sickle cell.
Kwa
wakina mama wenye sickle cell na wenye mpango wa kubeba ujauzito ni
vema wakafahamu kwamba upo uwezekano wa mtoto kudumaa kiakili akiwa
tumboni, kutoka ghafla kwa mimba na kupata kifafa cha mimba. Pia ni
vizuri kwa wagonjwa wa aina hii kutiwa moyo.
KUTOKA: http://ringomoses.blogspot.com/2008/01/ugonjwa-wa-seli-mundu-sickle-cell.html
No comments:
Post a Comment