Kuwashwa sehemu ya haja kubwa au katika ngozi inayozunguka sehemu hizo ni tatizo ambalo huwapata watu wengi wengi mara kwa mara na husababishwa na maambukizi, uchafu, baadhi ya vyakula na au kuumia ambavyo husababisha mtu kujikuna sana.
NINI USABABISHA?
Tatizo ili usababishwa na mambo mengi kama:-
Kuwashwa kwa ngozi, hii hutokana na unyevunyevu, toileti pepar, maji na mafuta yanayotumika kusafisha njia hii.
Kasoro katika mfumo wa chakula, kama kuharisha kwa muda mrefu au kukusa haja kubwa.
Uvimbe katika njia ya aja kubwa, ambapo kuwashwa huwa ni dalili kuu ya uvimbe katika njia ya haja kuu
Maambukizi, kama magonjwa ya zinaa kwa wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile, minyoo kwa watoto na watu wazima au maambukizi ya fangasi kwa wanawake
Magonjwa ya ngozi, kama psoriasis, vipele na saratani katika njia hii pia huweza kusababisha muwasho.
MATIBABU YAKE.
Tatizo ili hutibiwa kutokana na nini kilichosababisha ambapo kubadili vyakula, usafi, dawa na upasuaji huweza kufanywa ili kuondoa tatizo ili:-
DAWA, dawa za hydrocortisone, Desitin, Balmex, Antihistimine antibiotic na dawa za minyoo huweza kutumika kutokana na kisababishi cha tatizo ili. kumbuka lisipopona kwa muda wa wiki 2 unapaswa kwenda hospitali kwa uchunguzi zaidi.
USAFI, hakikisha unavaa nguo ya ndani iliyokauka, safisha na kausha njia hii baada ya haja kubwa, usikune njia hii kama una muwasho, na usivae nguo za kubana.
UPASUAJI, hii ufanywa hosipitali kama kuna uvimbe au kovu, au saratani ili kuondoa tatizo.
No comments:
Post a Comment