- Tibu magonjwa kwanza, hii ni endapo harufu mbaya itakuwa inasababishwa na maambukizi au magonjwa sugu kama meno kuoza, matatizo ya fizi, vidonda mdomoni,magonjwa ya mfumo wa hewa na chakula kwa kutumia dawa utakazoelekezwa hospitali.
- Piga mswaki, asa unapoamka na baada ya kula. Kumbuka kutumia mswaki laini na dawa yenye madini ya fluoride ili kuyapa meno afya bora na kuzuia harufu mbaya. Usisahau pia kusafisha ulimi.
- Sukutua mdomo mara kwa mara, kwa kutumia vinywaji laini au maji safi itakusaidia kuondoa mabaki ya chakula ambayo husababisha harufu mbaya.
- Epuka midomo kuwa mikavu, kwa kupunguza uvutaji wa sigara, tumbaku, unywaji wa pombe. Kunywa maji mengi, kula matunda, kunywa maji mengi, tafuna bigiji na lamba pipi zenye sukari kiasi ili kulainisha midomo yako iwe na unyevu muda mwingi.
- Epuka vyakula vinavyosababisha, kama vile vinavyonata, vyenye sukari nyingi, na kutafuna vitunguu au vitunguu swaumu.
- Badili mswaki walau mara moja kwa miezi mitatu mpaka minne.
- Muone Daktari wa meno na kinywa walau mara moja kwa mwaka kwa uchunguzi na matatizo madogo madogo.
Sunday, 17 August 2014
JINSI YA KUONDOA HARUFU MBAYA MDOMONI.
Harufu mbaya ya kinywa husababisha mtu kuwa na hofu au aibu mbele za watu. Hii husababishwa na baadhi ya vyakula, uvutaji wa sigara na tumbaku, midomo kuwa mikavu, kutofanya usafi au maambukizi mbalimbali katika njia ya hewa na chakula.Yafuatayo ni mambo unayoweza kufanya ili kuondoa au kupunguza harufu mbaya mdomoni:-
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment