Tuesday, 26 August 2014

MAMBO YA KUFANYA KILA UAMKAPO ASUBUHI

Kwa kawaida mida ya asubuhi huwa ni rafiki mkubwa kwa binadamu kwani uamka ukiwa na akili mpya ili kuanza siku mpya. Haya ni mambo ambayo unapaswa kufanya pale uamkapo asubuhi ili kuboresha afya yako kwa kuepuka magonjwa ya moyo, akili, na kupata mafanikio katika maisha.

  • Kunywa glasi ya maji, itakusaidia kuondoa uchafu na sumu mwilini kupitia haja ndogo
  • Amka mapema,  toka nje na fanya mazoezi mepesi na nyoosha viungo walau kwa dakika 20 itasaidia kuchangamsha akili na kuongeza afya ya ubongo katika kutunza kumbu kumbu
  • Kunywa chai badala ya kunywa kahawa au kula matunda yenye nyuzinyuzi, au chakula kiasi chenye protein
  • Piga mswaki ili kuimarisha afya ya kinywa na kuzuia magonjwa katika mifumo ya hewa na chakula
  • Elekeza akili yako katika mafanikio na kusahau vikwazo na udhaifu wako, jisahihishe makosa na kuweka mipango endelevu.
  • Soma au tazama kitu chochote kinachokuvutia itakusaidia kutabasamu, kucheka au kusahau matatizo na kufanya kazi zako vizuri.
  •  Hakikisha unaaga kila unapotoka nyumbani asubuhi itakusaidia kupata baraka na kutuliza akili katika shughuli zako.


No comments:

Post a Comment

.