Sunday 3 August 2014

HUDUMA YA KURUDISHA MAPIGO YA MOYO NA UPUMUAJI



Huduma hii inaweza kutolewa wakati wowote na mtu yoyote ili kuokoa maisha ya mtu mwingine pale anapoanguka na kupoteza fahamu. Huduma hii huitajika haraka kurudisha mapigo ya moyo na upumuaji ili kuzuia hali ya ubongo kukosa damu na chakula na hatimaye kifo.

Majeruhi yumo hatarini endapo mapigo ya moyo yatasimama,kupoteza damu nyingi, na kama akiendelea kupoteza fahamu, ni dhahiri ulimi unaweza kulegea na kuziba njia ya hewa. Toa huduma ya kwanza ifuatayo: *Angalia hatari zilizopo katika mazingira ya tukio. *Mlaze chali na kumuita pamoja na kumtikisa kiasi endapo ataonyesha dalili ya uhai, kama kushtuka, kupepesa macho au hata kuitikia. *Kama hana dalili ya hizo, muangalie kama anapumua kwa kumbinua kichwa nyuma ukiinua kidevu chake na kusikiliza mguso wa pumzi zake. *Kama hapumui, ita msaada haraka kabla hujaendelea na hatua nyingine. *Angalia kwa haraka mapigo ya moyo kwa kubonyeza mshipa mkuu shingoni chini ya shavu. Kama hakuna: *Mtoe takataka haraka kinywani kama anazo. *Mbonyeze moyo kifuani kwa kina cha sentimita mbili na nusu mara thelathini, na kumpa hewa mapafuni kwa njia ya mdomo kwa mdomo ukibandika mdomoni mwake kipande chembamba cha plastiki au kifananacho chenye tundu kuepusha maabukizi unapopitisha hewa. Utafanya hivi mpaka atakapoanza kupumua mwenyewe, utakapopata msaada wa kupokelewa, au umechoka kabisa na uko peke yako. Kwa utaratibu huu unaweza kuokoa uhai wa majeruhi.

No comments:

Post a Comment

.