UONAPO DALILI HIZI USIPUUZE ZINAWEZA KUPELEKEA KIFO.
Mara nyingi mwili wa binadamu hutoa dalili na ishara kuonyensha kuwa kuna kasoro inayoendelea kutokana na magonjwa au tatizo lolote la kiafya ambapo wengi wetu hatuchukulii kiundani ishara hizi na kuuacha mwili ufanye kazi na kukabiliana na kasoro wenyewe. Kuna baadhi ya dalili huwa ni hatari sana hivyo hupaswi kudharau wala kupuuza bila kufika kituo cha afya au hospitali.
- Dalili na Ishara za kiharusi,kama mwili kuwaka moto, ganzi, kusisimuka, kupooza mikono na miguu, kuchanganyikiwa, kuona vitu mara mbili mbili, kizunguzungu, kushindwa kuongea vizuri na mwili kuwa dhaifu upande mmoja. Usipuuze dalili hizi wahi hosipitali mapema kabla haijafikia hatua ngumu ya kutotibika na kusababisha kifo.
- Dalili na ishara za Pumu ya papo, huwa na dalili na ishara hatari kama mapigo ya moyo kwenda mbio, kupumua kwa shida, kutoa sauti kama miluzi, kukooa sana na kifua kubana sana, wai hospitali ili kupata huduma mapema ili kuepuka kifo kitakachosababishwa na kuongezeka kwa hewa ya Carbondioxide katika damu na upungufu wa oxygen na hivyo kuharibu ubongo na mfumo wa upumuaji.
- Dalili na ishara za shambulio la moyo, kama maumivu makali ya kifua, mikono, shingo na taya, uchovu mwingi, kichefuchefu, kutapika, kukosa nguvu, na kutokwa na jasho kali kipindi cha baridi.Upatapo dalili hizi wasiliana na wataalamu wa afya mapema watakaokuelekeza dawa kwa ajili ya kulinda na kurekebisha mapigo ya moyo na kulinda mishipa na misuli ya moyo.
- Dalili na ishara za mtu kujinyonga, usipuuze unapoona dalili hizi ni hatari sana kama msongo wa mawazo, uchungu, huzuni, masikitiko, uchovu wa muda mrefu, kutojali, wasi wasi, kukosa usingizi na hamu ya kula na kujifikiria vibaya.Unapaswa kuwasiliana na madaktari au wataalamu wa saikolojia au ndugu wa karibu.
- Dalili ya kuvuja damu katika ubongo, hizi hutokea ghafla kama maumivu makali ya kichwa, kupoteza fahamu, kuona mawenge, kutapika na kifafa.
- Dalili za kukojoa au kukooa damu, usipuuze dalili hizi zinaweza kuwa ishara za mwazo wa saratani katika mapafu, kibofu, figo, mirija ya mkojo au maambukizi ya wadudu na vimelea hatari sana.
No comments:
Post a Comment