Wednesday 6 August 2014

DAWA ZA NYWELE ZINAVYOSABABISHA UVIMBE KATIKA KIZAZI

Dawa za kulinisha nywele (relaxer) zimekuwa zinapendwa na wanawake wengi wa Afrika kwa kuwa zina uwezo wa kulainisha nywele na kumfanya apendeze na awe wa kuvutia.
Hata hivyo, wataalamu wa afya wanadai kuwa dawa hizo zinasababisha uvimbe kwenye kizazi kutokana na kemikali za dawa hizo ambazo huingia mwilini kupitia majeraha au ngozi wakati wa kupaka.


Pia dawa za nywele na vipodozi zina kemikali ambazo husababisha uzalishwaji wa vichocheo kwa kiasi kikubwa na kusababisha uvimbe kwenye kizazi uitwao fibroids au leimyoma.
Kemikali hizi hupenya kwenye ngozi na wakati mwingine hata kwa harufu tu, husababisha kuzalishwa kwa wingi wa vichocheo aina ya estrogen ambavyo huchangia kuota kwa uvimbe wa fibroids mara nyingi kabla mwanamke hajaacha kuzaa. 
PANGA JINSI YA KUPATA MTOTO WA KIUME 
Baadhi ya dawa za nywele husababisha matatizo ya upumuaji, tumbo, kuunguza fuvu, nywele kukatika na kunyonyoka au kupoteza nywele moja kwa moja hivyo inakupasa kupata ushauri au kusoma maelekezo kabla ya kuchagua aina bora ya dawa kutokana na nywele zako.


No comments:

Post a Comment

.