Kijana huyo wa miaka tisa Kieran Sorkin alizaliwa bila masikio na madaktari wamekuwa wakifanya majaribio ya mbinu mpya ya matibabu katika hospitali ya Great Ormond Street iliyoko jijini London..
Kieran aliyezaliwa kama kiziwi hakuwa na masikio alipozaliwa badala yake alizaliwa na shimo mbili na ndewe tu badala ya masikio.
Tayari kieran anasikia baada ya upasuaji wa awli ambao ulimsaidia kupandikiza kifaa kinachomsaidia kupaza sauti ndani ya masikio yake.
"Ningependa watu wakome kuniuliza kwanini unakaa tofauti hivi ", alisema Kieran akiwa katika mtaa wa Hertfordshire.
"nimefurahishwa sana kufanana na marafiki wangu ''.
"Hata mimi ninafurahi kuwa sasa nitaweza kuvaa miwani na vifaa vya kusikizia muziki."
SOMA ZAIDI http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/08/140812_boy_ears_created_from_ribs.shtml
No comments:
Post a Comment