Thursday 21 August 2014

TATIZO LA MIGUU NA MIKONO KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI.


Katika mwili wa binadamu, kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto na kufa ganzi kwa viungo vya pembezoni mwa mwili kushindwa kushika au kunyanyua kitu, kuchoka kwa misuli na kadhalika.Matatizo haya ya kiafya (miguu/mikono kuhisi ganzi, baridi au maumivu) husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili (miguuni au mikononi) na
hivyo kupoteza uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika, miguuni au mikononi.
Miongoni mwa mambo ambayo hupelekea neva hizi za pembezoni kudhoofika na kushindwa kufanya kazi vizuri ni haya yafuAatayo:

  • Kupungua kwa virutubisho mwilini,hasa mkusanyiko wa vitamini B,(Vitamin B Complex).
  • Matumizi ya dawa, mfano dawa za kutibu kifua kikuu au za kupambana na virusi vya ukimwi
  • Uzito mkubwa wa mwili.
  • Ugonjwa wa kisukari(diabetic neuropathy).
  • Shinikizo la damu.
  • Unywaji wapombe kupita kiasi
  • Magonjwa ya figo.
Ili kuzuia tatizo ili fanya mazoezi,kula vyakula vyenye virutubisho, kula mboga mboga na matunda, chua miguu yako kila siku, punguza pombe pombe na sigara na fanya mazoezi kiasi kuondoa tatizo ili..

No comments:

Post a Comment

.