Tuesday 12 August 2014

ZMAPP DAWA YA KUTIBU EBOLA

Jopo la wataalam wa shirika la afya duniani WHO limeamua kwamba watu wanaweza kutumia dawa ambazo hazijajaribiwa katika mwili wa binaadamu kutibu ugonjwa wa ebola,iwapo maagizo fulani yataheshimiwa ikiwemo ruhusa ya mgonjwa.

Tangazo hilo linajiri huku shirika hilo likitangaza kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo imepita watu 1000 na kwamba kasisi wa uhispania aliyeondolewa nyumbani mwake baada ya kuambukizwa ugonjwa huo amefariki.

Dawa hiyo ambayo haijajaribiwa imetumiwa na raia wawili wa kutoa msaada kutoka marekani ambao afya yao imeimarika,lakini kasisi huyo wa Uhispania ambaye pia aliitumia dawa hiyo ameaga dunia.
Watu wasiopungua 1,013 wameaga dunia kutokana na kuambukizwa virusi hivyo katika ukanda wa Afrika Magharibi.
Hatua hii ilichukuliwa huku Liberia ikitangaza kuwa ilihitaji kupata dawa la kufanyia majaribio liitwalo Zmapp baada ya kuiomba serikali ya Marekani.
Shirika la WHO lilisema kuwa lilikuwa limeombwa kupendekeza hatua hiyo kwa sababu ya kusambaa kwake na idadi kubwa ya vifo
SOMA ZAIDI http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/08/140812_ebola_zmap_liberia.shtml

No comments:

Post a Comment

.