Wednesday, 6 August 2014

MADHARA YA KUKOSA USINGIZI KWA MUDA MREFU

Kukosa usingizi na kutokulala vizuri mara kwa mara husababisha matatizo mengi kiafya katika muonekano, kumbukumbu, ngozi, uzito, akili na usalama katika mazingira. Yafuatayo ni matatizo ambayo unaweza kuyapata endapo utakosa usingizi mzuri kwa muda mrefu au kulala vibaya.

  • Ajali, kukosa husingizi kwa muda mrefu usababisha uchovu ambao unaweza pelekea kuumi katika mazingira na kazini.
  • Kuharibu uwezo wa kufikiria, hupunguza akili ya mtu kufikiria, kujifunza, kukumbuka vitu kwa haraka na kufanya maambuzi sahihi ya vitu.
  • Hatari ya kupata magonjwa, kukosa usingizi mara kwa mara umuweka mtu katika hatari ya kupata magonjwa ya akili, moyo, presha, kiharusi, kisukari nk.
  • Kukosa hamu ya mapenzi, hii ni kwa wote wake kwa waume kwani uharibu mfumo mzima wa mapenzi na hormoni katika mwili na kupunguza au kumaliza hamu ya kufanya mapenzi.
  • Msongo wa mawazo, kukosa usingizi kwa muda mrefu usababisha huzuni, kufadhaika, maumivu ya kichwa, wasi wasi  kukosa raha na amani asa kwa wale wanaolala chini ya masaa 6 kwa siku.
  • Kuzeesha ngozi, kukosa usingizi kwa muda mrefu usababisha ngozi kuwa na mikunjo, kubadilika rangi na kuzeeka na macho kuvimba. 
  • Kuongezeka uzito, kwa kuongeza njaa na hamu ya kula ukufanya kuwa na uzito kupita kiasi.
WASILIANA NASI KWA MSAADA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

.