Monday 18 August 2014

JINSI YA KUMKINGA MWANAO NA POLIO

Polio hutokea zaidi kwa watoto walio na umri chini ya miaka miwili. Ugonjwa huu unaosababishwa na vijidudu vya virus, huanza kama mafua, homa, kutapika na maumivu ya misuli kwa mtoto.
Mara nyingine, hizi ndizo dalili zinazoonekana tu. Lakini, wakati mwingine sehemu fulani ya mwili hulegea au kupooza. Mara nyingi hii hutokea kwenye mguu au mkono mmoja. Baada ya muda mguu au mkono uliopooza huwa mwembamba na haukui kwa haraka kama huo mwingine.

TIBA:
Ikiwa ugonjwa umekwishaanza hakuna dawa itakayoweza kuondoa kupooza. Dawa za kuua vijidudu hazisaidii. Tuliza maumivu kwa asprini au Astaminofeni na kukanda misuli inayouma kwa maji moto.

KINGA:
Mweke mtoto mgonjwa kwenye chumba tofauti mbali na watoto wengine. Mama ni lazima anawe mikono kila mara baada ya kumgusa. Kinga iliyo nzuri kuliko zote kwa polio, ni chanjo ya polio.
Hakikisha kuwa watoto wamezindikwa kuzuia polio kwa matone akiwa na umri wa miezi miwili, mitatu na minne.
Mtoto aliyelemazwa na polio ni lazima ale chakula bora na kufanya mazoezi ili kuipa nguvu misuli iliyobaki. Kwa mwaka wa kwanza, nguvu inaweza kurudi kidogo.
Msaidie mtoto ajifunze kutembea kwa jinsi anavyoweza. Weka nguzo mbili ili aweze kuegemea. Baadaye, mtengenezee magongo ya kutembelea.

IMETOKA BUGANDO HEALTH MOVEMENT

No comments:

Post a Comment

.