Saturday 16 August 2014

MATUMIZI SAHIHI YA PEDI ILI KUEPUKA MADHARA.


Wanawake wanashauriwa kufanya yafuatayo ili kuhakikisha usalama wa afya zao watumiapo pedi :

1. Kunawa mikono vizuri kwa sabuni kabla ya kugusa pedi ambayo unatarajia kuivaa na baada ya kuvaa kunawa tena mikono vizuri.

2. Kutohifadhi pedi bafuni au chuoni au sehemu yote yenye unyevunyevu na isiyo na mwanga wa kutosha ili kutotengeneza mazingira ya kukua kwa vimelea vya magonjwa ndani ya pedi.

3. Kuangalia kwa makini muda wa matumizi ya pedi kabla ya kununua au baada ya kutunza pedi kwa muda muda mrefu ili kuepuka kutumia pedi zilizopita muda wake wa matumizi.

4. Kuepuka kununua pedi zinazouzwa kiholela na zisizothibitishwa na TBS na mamlaka nyingine zenye dhamana ya kuangalia ubora wa pedi hizo. Mwanamke anatakiwa kuangalia nembo ya uthibitisho wa mamlaka hizo na kujiridhisha kuhusiana na usalama wa pedi hizo kabla hajanunua.

5. Kubadilisha pedi kila baada ya masaa mawili, kama tunavyojua damu ni moja wapo ya chakula kizuri sana kwa vimelea vya magonjwa kama bacteria ,unyevunyevu unaosababishwa na kuvaa pedi kwa muda mrefu pia unapelekea ustawi wa bacteria hao na joto ambalo lipo katika maumbile ya ndani ya mwanamke vikiungana kwa pamoja vinatengeneza mazingira mazuri ya ukuaji wa bacteria , hivyo wanawake wanashauriwa kutovaa pedi hizo kwa muda usiozidi masaa mawili ili kuepuka mazingira hayo.

6. Kuchagua aina sahihi inayokutosha ina kuepuka pedi zinazobana sana kupita kiwango sababu zinaweza pia kukufanya usiwe huru na kutengeneza joto la ziada na michubuko katika maumbile ya mwanamke,hivyo mwanadada unashauriwa kutumia pedi itakayokukaa vizuri(isilegee sana wala kuachia sana)

7. Kwa wadada wanaotumia vitambaa badala ya pedi ni muhimu pia kuzingatia kanuni za kiafya na usafi kabla na baada ya kutumia vitambaa hivyo kama vile kuchagua kitambaa angavu ,kukiloweka na kukifua vizuri, kuanika kwenye sehemu yenye mwanga wa jua wa kutosha na upepo wa kutosha pasipo na unyevunyevu ,kupiga pasi kabla ujakihifadhi na kabla ya kutumia ili kuuwa vimelea vya magonjwa

No comments:

Post a Comment

.