Tuesday 12 August 2014

TATIZO LA KUWASHWA LIPS NA TIBA YAKE

Hili ni tatizo ambalo mtu uhisi kuwashwa na kuwa na hamu ya kujikuna ngozi au kuvimba sehemu za mdomo(Lips). Hii husababishwa na vipodozi, lipsticks, vyakula, mazingira na magonjwa mbalimbali asa malengelenge, magonjwa ya ngozi, chango, saratani, kuchafuka kwa damu, ukurutu, matatizo katika nyongo, ukosefu wa vitamini nk.


MATIBABU YAKE.
Unaweza kujitibu tatizo hili kwa kuepuka aina ya vyakula, vipodozi na lipsticks ambavyo hujawahi kutumia. Pia unaweza kutumia dawa zinazoongeza vitamins kama Multivitamin complex au kula vyakula vyenye vinavyoongeza vitamin mwilini sambamba na kulainisha lips. Kumbuka kujikuna au kugusa sehemu inayowashwa itakupelekea kukuza tatzo na kuongeza maambukizi mengine.
Kama tatizo haliponi unaweza kufika hospitali au kituo chochote cha afya kwa uchunguzi ambapo dawa kama cetrizene, hydrocortisone, acyclovir, antibiotics kwa njia ya sindano, vidonge au cream huweza kutolewa kutokana na ukubwa wa tatizo.

1 comment:

  1. Huwa nawashwa mdomo na naijsikia kujikuna mala nyingi sehem ya juu ya mdomo na hata dk1 haiishi huwa nashtuka kushavimba ata nisipokuna inavimba tatizo linaweza kua nin?

    ReplyDelete

.