Mwili wa binadamu ni kama mashine umri unavyozidi kwenda basi viungo navyo vinachoka. kutokana na uzito maumivua haya uanzia kwenye miguu kutokana na kuvimba na kujaa maji kwenye jointi au kukosa vilainisha. Hali hii usababisha maumivu makali kwenye misuli, mifupa, jointi, mwili kuwa dhaifu, kukosa usingizi na kushindwa kutembea.
MATIBABU YAKE
Haya matatizo tunaweza kupunguza kwa kujenga tabia ya kufanya mazoezi
kila siku na kula lishe bora na yenye protini, kalisium na vitamini D kwa wingi. Tujenge tabia ya kukimbia au kutembea kila
siku japo kwa dakika 30 na tuwakumbushe wazee wetu pia au tuwachukue
tufanye nao mazoezi haya kwa pamoja kama tunaishi nao majumbani kwetu.
Pia unaweza kuwasiliana na wataalamu wa afya kwa ajili ya kupata dawa za kupunguza au kuondoa maumivu, uvimbe, au kuunganisha mifupa kama itakuwa imevunjika au kuwekewa vifaa vya kulinda jointi zako.
No comments:
Post a Comment