PIA MADHARA YA KUKOSA USINGIZI
- Uvutaji wa Sigara, kwa kawaida wagonjwa wengi wa kikohozi cha muda mrefu huwa ni wavutaji wa sigara na baadhi hupona pale wanapoacha na wengine huchelewa baada ya kuwa wamepata matatizo mengine makubwa katika njia ya hewa.
- Ugonjwa wa pumu, ambapo njia ya hewa uvimba, kujaa maji na kuzuia mfumo wa upumuaji kufanya vizuri.
- Ugonjwa wa kucheua na kiungulia(Gastro esophageal reflux disease) hii usababishwa na chakula ambacho kishaingia tumboni na kuchanganywa na tindikali kurudi kaika koo na hutokea mara nyingi usiku ambapo mtu hushindwa kupumua vizuri na kukooa sana.
- Kuvimba mianzi ya pua, ambapo mtu uhisi kitu, kutekenywa au kuwashwa kooni na kukooa kwa muda mrefu.
- Maambukizi, ambayo husababishwa na bakteria na virusi katika njia ya hewa kama pnemonia, kifaduro, na magonjwa mengine ya moyo na mapafu.
- Matatizo mengine ambayo husababisha mara chache ni pamoja na Allergy, dawa za muda mrefu, saratani, TB, emphysema, mapafu kuanguka.
WASILIANA NASI KWA MSAADA ZAIDI
No comments:
Post a Comment