Sunday, 3 August 2014

MADHARA YA VIDONGE VYA KUZUIA MIMBA

Vidonge vya kuzuia mimba huwa na hormoni za estrojeni na projesteroni zilizotengenezwa kwa ajili kuzuia hutoaji wa yai kutoka kwenye ovari kwa. Mara nyingi dawa hizi hutumika kuanzia siku ya tano ya mzungungo wa hedhi kwa muda wa siku 21 na huwa na madhara yafuatayo kwa mtumiaji




  • Msongo wa mawazo na hasira
  • Kipandauso na maumivu ya kichwa
  • Kupoteza hamu ya kufanya mapenzi
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Kuongezeka uzito
  • Tumbo kuvimba na kujaa gesi
  • Nyongo kujaa mawe
  • Homa ya manjano
  • Kukosa hedhi au kuwa na mzunguko usio kawaida
  • Kutokwa na usaa au damu sehemu za siri
  • Uvimbe katika kizazi
  • Maziwa kuuma
  • Maumivu ya miguu
  • Mabaka mabaka usoni
 Pamoja na kuwa na madhara haya vidonge hivi bado ni muhimu kwa ajili ya uzazi wa mpango hivyo ni muhimu kuwasiliana na wataalamu wa afya kabla ya kutumia ili kutambua matumizi sahihi na muda wa kuanza na kuacha matumizi ya vidonge hivi kabla ya kusababisha madhara makubwa zaidi


No comments:

Post a Comment

.