- Jaribu kutumia sahani ndogo, na usichote chakula mara ya pili (usiongeze), watafiti wameona kwamba mtu anayetumia sahani kubwa mara nyingi anakula chakula kingi kuliko akitumia sahani ndogo.
- Nusu au zaidi ya mlo uliochotea kwenye sahani iwe ni vyakula vinavyotokana na mimea hasa mboga mboga. Kama unakula “sandwich” ya mkate, kula nusu na ongezea kwa mbogamboga na matunda.
- Asubuhi ule mlo wa kushiba zaidi na jioni ule chakula kidogo/chepesi (usishibe sana usiku).
- Usile kwa haraka, mara nyingi unapokula kwa haraka unakula chakula kingi na pia chenye nishati nyingi. Ongeza vyakula vyenye makapi mlo kwa wingi kama mbogamboga, nafaka zisizokobolewa (whole-grains), mara nyingi vyakula hivi huwezi kula haraka wala huwezi kula kupita kiasi.
- Jipe muda wa kutosha kutafuna vizuri, na mara nyingi vyakula bora kama ugali wa dona, mkate wa brauni, mahindi ya kuchoma au kuchemsha, maharage, kunde huhitaji kutafunwa vizuri hivyo huwezi kula kupita kiasi.
- Epuka asusa zenye mafuta mengi, sukari nyingi au chumvi nyingi. Jizoeshe matunda, hindi la kuchoma au vyakula vingine vya aina hiyo.
- Jipe muda kujitayarishia mlo ulio bora wenye mboga mboga nyingi. Kumbuka ni uhai wako. Labda umetumia dakika 10 zaidi kutayarisha mlo lakini imekuepusha kutumia siku nzima au zaidi kwa daktari na kulipa gharama kubwa.
- Epuka kutumia vyakula vilivyotengenezwa kwa haraka (fast food) kwenye migahawa, mara nyingi vina mafuta mengi, chumvi nyingi au sukari nyingi. Na pengine unaona umekula asusa (snack) tu, kwa hiyo unakula tena mlo mzima. Kwa mfano watu wengine husema “I grabbed something” kwa maana hajala vizuri kumbe ni kwa kuwa alikula bila mpango.
- Epuka kula ukiwa unaangalia TV, unatumia computer au unafanya shughuli nyingine kwani una hatari ya kula kupita kiasi.
- Tuwazoeshe watoto ulaji bora unaoshirikisha mbogamboga na matunda, na aina za kunde, nyama kwa kiasi. Epuka kummzoesha chumvi nyingi, mafuta mengi au sukari nyingi. Akishazoea itakuwa shida kuacha. Mpende mwanao, mfundishe vitu vitakavymrefushia maisha.
- Epuka pombe na sigara
- Fanya mazoezi ya mwili angalau dakika 30 au zaidi kila siku, hata kutembea tu.
- Kumbuka mwili wako unatokana na unachokula na mazoezi unayofany
Saturday, 9 August 2014
KUPUNGUZA UZITO UKUSAIDIA KUPAMBANA NA MAGONJWA HAYA SUGU.
Uzito uliozidi kiasi unakuweka kwenye hatari ya kupata magonjwa mengi
sugu kwa mfano, kisukari, msukumo mkubwa wa damu, magonjwa ya moyo,
figo, saratani na mengineyo. Magonjwa haya yanaleta kifo mapema na
matatizo mengine mengi…. Jizoeshe taratibu za kula ambazo zitakusaidia
kupunguza uzito au kuzuia ongezeko kubwa la uzito..Badili mtindo wa
kula, yafuatayo yanaweza kukusaidi:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment