- Punguza kiasi cha chumvi, hii itakusaidia kushusha presha na hivyo kuepuka matumizi ya dawa. kumbuka sio tu chumvi ya kuweka kwenye chakula bali hata vyakula vinavyouzwa vimeandaliwa tayari huweza kuwa na chumvi kiwango kisichostahili. unaweza kutumia viungo tofauti vya kuongeza ladha ya chakula kama chili, limao, na tangawizi.
- Kula sana matunda na mboga za majani, jitahidi kula walau matunda zaidi ya matano kwa siku itasaidia kupunguza presha. Epuka matunda na mboga za majani vilivyotengenezwa na kuongezewa chumvi, mafuta na sukari.
- Punguza uzito, kupunguza uzito kwa kufanya mazoezi, kupunguza mafuta na na vyakula vinavyoongeza nguvu pia itakusaidia kupunguza shinikizo la damu.
- Punguza kiasi cha pombe ikiwezekana acha kabisa, kupunguza au kuacha pombe pia itakusaidia kushusha presha kwa kiasi kikubwa.
- Fanya mazoezi, kufanya mazoezi ya kawaida walau dakika 30 kwa wiki itakusaidia kupunguza presha na hivyo kupunguza madhara.
Sunday, 17 August 2014
UNAWEZA KUSHUSHA PRESHA KWA KUFANYA HAYA
Mitindo ya maaisha tunayoishi na vyakula tunavyokula hutuweka katika hatari ya kusumbuliwa na shinikizo la damu(Presha). Hii hutokea pale presha inapoongezeka zaidi ya 120/80. Yafuatayo ni mambo unayoweza kufanya ili kupunguza presha na hivyo kuepuke hatari ya kupata shambulio la moyo, kiharusi na figo kushindwa kufanya kazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment