Monday 18 August 2014

JITIBU MWENYEWE MAUMIVU YA KIFUA

Maumivu ya kifua usababishwa na matatizo mengi mwili ambapo mengi huwa ni madogo na hayana madhara sana mwilini ila usababisha usumbufu. sana kwa muhusika. Mara nyingi maumivu ya kifua husababishwa na matatizo katika moyo, mapafu, koromeo, mbavu, na kuziba kwa ateri zinazosambaza damu sehemu za mwili na moyo. Endapo unasumbuliwa na maumivu ya kifua kwa muda mrefu au ya papo hapo jaribu kufanya yafuatayo:-

  •  Epuka mazingira ya baridi au joto kali.
  • Fanya mazoezi laini kama ulivyoelekezwa na daktari
  • Epuka kazi ngumu ambazo husababisha au kuongeza maumivu ya kifua
  • Kula lishe bora kwa mpangilio na epuka vyakula vya vyakula vyenye mafuta.
  • Punguza uzito na pata muda mwingi wa kupumzika au kukaa mkao unaopunguza maumivu
  • Usinywe pombe au kuvuta sigara na tumbaku kupita kiasi
  • Punguza mawazo na hasira kwa kufanya mabo yanaondoa matatizo haya.
  •  Maumivu yakizidi nenda hospitali ambapo utapewa dawa kama  Nitroglycerin, na paracetamol kwa ajili ya kupunguza maumivu kwa maelekezo ya wataalamu wa afya.
  • Pumua kwa kasi ukitolea hewa mdomoni na kuingiza hewa puani itakusaidia kupunguza maumivu haya.
  • Epuka makelele na pumzika ndani na ikiwezekana fumba macho na waza mambo mazuri tu au ongea na rafiki au jamaa.
  • Lala chali na mikono weka kichwani itakusaidia kufungua mapafu na kuruhusu hewa ya kutosha.
 


No comments:

Post a Comment

.