Monday 4 August 2014

ATHARI ZA MVINYO KWA AFYA YAKO.

Pamoja na kutumiwa kupunguza uchovu, kusaidia mmeng'enyo wa chakula, kuharisha, kutapika na kuzuia maumivu watafiti wanadai kuwa mvinyo mwekundu (Red wine) hauna manufaa kama ilivyodhaniwa kuwa nayo kwa moyo wa binadamu pale unapotumiwa mara kwa mara na kupita kiasi kama ifuatavyo.

  • Kudhoofisha mifupa, utumiaji wa pombe muda mrefu usababisha kudhoofika na kuvunjika kwa mifupa kwa kuathiri cell ambazo hutengeneza mifupa.
  • Kansa, hutumiaji wa wine kupita kiasi au kwa muda mrefu husababisha hatari ya kupata saratani ya koo, tumbo, utumbo, mapafu  na maziwa,
  • Kuhathiri mfumo wa damu, utafiti unaonyesha kuwa unywaji wa mvinyo kupita kiasi husababisha magonjwa ya moyo, mishipa na damu kwa kubadili mapigo ya moyo na kupunguza kolesteroli ambazo hurekebisha mzunguko wa damu
  • Matatizo ya akili, hutumiaji wa wine kwa muda mrefu uharibu uwezo wa akili asa katika tabia, kumbukumbu na uwezo wa kutambua vitu kwa kuharibu seli katika ubongo.
  • Ugonjwa wa kisukari, unywaji wa pombe kupita kiasi usababisha kuongezeka kwa sukari mwilini wakati unywaji wa kawaida hupunguza uwezekano wa kupata kisukari.
  • Maumivu ya kichwa, hii hutokana na kupoteza maji mengi na kemikali zilizo katika mvinyo kama histamine, serotonini kama inavyoonekana katika hangover.

No comments:

Post a Comment

.