Monday, 4 August 2014

DALILI NA MATIBABU YA MINYOO

 Mnyoo ni aina ya nematodi mkubwa ambaye anaishi katika matumbo ya Binadamu na anasababisha ugonjwa wa minyoo.
 Inakadiriwa kwamba karibu ya robo ya idadi ya watu duniani wameathiriwa na ugonjwa huu, na hasa umeenea sana katika maeneo ya kitropiki na maeneo yenye hali duni ya usafi. 

Aina nyingine ya minyoo ya jamii ya Askaris inaweza kusababisha magonjwa katika mifugo.
Maambukizi hutokea kwa njia ya kula chakula kilichoathiriwa na kinyesi chenye mayai ya minyoo aina ya Askaris. Buu wa mnyoo hutotolewa, na kujichimbia kupitia utumbo mdogo, hupita mpaka kwenye mapafu na mwishowe kufikia na kuhamia katika mfumo wa hewa. Kutoka hapo humezwa na mtu na hurudi tena na hukua na kukomaa katika utumbo kwa kuongezeka hadi sentimita 30 (inchi 12) kwa urefu na hujishikiza katika ukuta wa utumbo.

DALILI
Kama idadi ya minyoo ni ndogo, unaweza kutoona dalili za ugonjwa huu. Hata hivyo unaweza kuambatana na:-
  • Homa
  • kuharisha
  • kuvimba tumbo
  • kuvimba ini au wengu 
  • Kichomi cha mara kwa mara
  • Kichefuchefu na kutapika minyoo ya duara
  • Maumivu ya tumbo
  • Kupungua uzito
  •  Matatizo mazito yanaweza kujitokeza kama minyoo itahamia sehemu nyingine za mwili kama mapafu, ini, na sehemu nyingine za mwili asa msokoto na kuoza kwa sehemu ya utumbo mdogoambayo hupelekea kifo.
MATIBABU
Dawa zinazotumika kuua nematodi huitwa kiuaminyoo ni pamoja na Mebendazole, ivermectin, Albendazole na Pyrantel pamoate ambazo hutolewa hosipitali kwa maelekezo ya daktari kulingana na ukubwa wa tatizo.
Kumbuka matumizi ya vyoo, ulinzi wa chakula kutoka uchafu na udongo na kuosha mkono kabla ya kula ni njia mojawapo za kujiepusha na magonjwa ya minyoo.

3 comments:

  1. Asante kwa elimu ya minyoo na madhara yake endelea kutujuza zaidi
    Je kuna madhara kutumia dawa za minyoo kabla ya kupima?

    ReplyDelete

.