Wednesday 13 August 2014

DALILI NA MATIBABU YA TETE KUWANGA

Tete kuwanga au Chicken pox  ni ugonjwa ambao uambukiza nakusababishwa na virusi vinavyojulikana kama Varicella zoster. Maambukizi ya tete kuwanga huonekana sana kwa watoto wadogo ingawa hata watu wakubwa pia hupata maambukizi ya ugonjwa huu. Tete kuwanga hupatikana duniani kote asa katika nchi zenye kupata majira ya baridi. Tete kuwanga huambukizwa kupitia njia ya hewa au kugusana mwili na mgonjwa wa tete kuwanga(kupitia majimaji yanayotoka kwenye vipele vya mgonjwa au anapokohoa.


 Dalili na viashiria vya Tete kuwanga
Dalili za kwanza ni;
• Kichefuchefu
• Kupungua kwa hamu ya kula
• Maumivu ya kichwa
• Maumivu ya misuli
• Kuumwa tumbo

Dalili hizi baadae hufuatiwa na hatua ya mgonjwa kutoka vipele, uchovu na homa ambayo sio kali sana, hatua hii ndio huonyesha kuwepo kwa ugonjwa wa tete kuwanga.

Vipele hivi mwanzo huonekana kama alama nyekundu ndogo kwenye uso, kichwa, tumbo,kifua, sehemu za juu za kwenye mikono na miguu ambapo baada ya masaa 10-12 alama zile nyekundu hugeuka kuwa uvimbe, uvimbe huu kisha hujaa maji na kupasuka. Baadae vipele vipya (blisters) huanza kuchipuka kwa makundi kwenye sehemu za tupu ya mwanamke (vagina), kope (eyelids) na mdomoni ambavyo hupasuka na kuwa vidonda vidogo vidogo kwenye sehemu hizi.

Hatua hii ya kutokea vipele huanza kuonekana kuanzia siku ya 10-21 baada ya mtu kupata maambukizi ya Varicella zoster virus na huambatana na kuwashwa sana mwili.Vipele vinaweza kutokea kwenye viganja vya mkono, nyayo na hata kwenye pua, lips, masikio, njia ya haja kubwa.

Vipele venye majimaji (blisters) hutokea siku ya 4-7 baada ya hatua ya kutoka vipele kuanza na hupotea kuanzia siku ya 5 na kuendelea.
Mtu ambaye ana maambukizi ya tete kuwanga huweza kuambukiza watu wengine siku moja au mbili kabla ya kuanza kutoka vipele na kuendelea kuwa na uwezo wa kuambukiza wengine kwa siku 4-5 baada ya vipele kutokea.

Dalili ya kwanza ya tete kuwanga kwa watoto ni vipele kabla ya dalili nyingine nilizotaja awali hapo juu kufuata.Kwa watu wakubwa, vipele husambaa katika maeneo mengi mwilini kwa wingi na homa huwa ya muda mrefu sana na pia huweza kupata homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Varicella zoster virus.


Baadhi ya watoto ambao walipata chanjo ya ugonjwa huu hapo awali huweza kupata tena maambukizi ya tete kuwanga ingawa yanakuwa sio makali sana(hutoka vipele 30 kwa wastani) lakini watoto hawa bado wana uwezo wa kuambukiza wengine ugonjwa huu.Kwa kawaida mtoto hutokea wastani wa vipele 250 hadi 500 wakati wa maambukizi ya ugonjwa wa tete kuwanga.


Ugonjwa huu ni nadra sana kuwa na madhara makubwa ingawa madhara huweza kuonekana kwa wagonjwa walio na upungufu wa kinga mwilini, wenye kuugua magonjwa sugu au wanawake wajawazito ambao hawakupata chanjo ya ugonjwa huu.


Matibabu
Matibabu ya ugonjwa huu yanalenga kupunguza athari za dalili na viashiria vya ugonjwa huu na si kuua virusi vinavyosababisha ugonjwa huu.
Matibabu ya tete kuwanga yanahusisha;
a) Kuwakata watoto kucha ili kuepusha kujikuna na hatimaye kukata vipele hivyo kuongeza kutokea kwa vipele mwilini
b) Dawa za maumivu kama paracetamol n.k
c) Antihistamines-Dawa za kupunguza kuwashwa mwili
d) Calamine lotion ingawa hakuna tafiti zilizofanyika kuthibitisha ubora wa matumizi yake dhidhi ya ugonjwa huu.Dawa hii ni salama
e) Kuongeza kiwango cha usafi wa mwili, kuosha mwili kwa maji ya uvuguvugu
f) Kukaa sehemu zenye baridi ili kupunguza kuwashwa mwili
g) Kuepuka kujikuna vipele
h) Dawa dhidhi ya virusi (antiviral medication) kama acyclovir au valacyclovir ambazo hutolewa saa 24-48 baada ya vipele kuanza,dawa hizi hupunguza kusambaa kwa virusi lakini haziui virusi hao.Dawa hizi hutolewa kwa wale ambao wana upungufu wa kinga mwilini na kwa wanawake wajawazito.Watoto chini ya miaka 12 au wale wenye umri wa zaidi ya mwezi mmoja hawaruhusiwi kutumia dawa hizi kama hawana tatizo la upungufu wa kinga mwilini ili kuwaepusha na madhara wanayoweza kupata kutokana na matumizi ya madawa haya.

No comments:

Post a Comment

.