Thursday 7 August 2014

UKOSEFU WA VITAMINI D UNAWEZA KUKUSABABISHIA UWENDAWAZIMU.

Ukosefu wa Vitamini D ambayo hupatikana
katika mionzi ya jua, maziwa, mayai, jibini na mafuta ya samaki hupunguza huwezo wa akili na ubongo kufanya kazi na kusababisha matatizo ya kisaikolojia kama uchizi, Alzemia na kuharibu kumbukumbu. Hii huwaathiri zaidi wazee, wavuta sigara, wasiofanya mazoezi, wanene kupita kiasi,  na wale wasiokula samaki na mboga za majani.

Pia husababisha matatizo ya mifupa ambayo unaweza kuyatambua kutokana na kuuma kwa viungo na mifupa au uchovu wa mara kwa mara, ngozi kuwa nyeusi kuliko kawaida na ukosefu wa vyakula tajwa hapo juu.
Katika ubongo na mfumo wa fahamu vitamini D husaidia kuongeza kasi ya neva kupeleka taarifa, kupunguza kalsiumu ambazo huweza kuleta madhara katika ubongo, kuongeza na kurekebisha kinga ya mwili, na kuondoa sumu mwilini.

No comments:

Post a Comment

.