Friday 15 August 2014

BANGI ILIVYOOKOA MAISHA YA MTOTO MDOGO

Mwanamke mmoja  Rachael Garner kutoka Florida anaamini bangi ndio iliokoa maisha ya mwanae mwenye umri wa miezi 19 baada ya madaktari kushindwa kumtibu matatizo ya kupooza ubongo na ubongo kujaa maji yaliyokuwa yakimsababishia ugonjwa wa kifafa.
Anaongeza kuwa baada ya kuambiwa kuwa mwanae huyo aitwaye Nettie alimuanzishia dozi ya bangi aina ya cannabidiol ambayo ilisaidia kupunguza dalili za tatizo alilokuwa nalo.
Kauli ya mama huyu inakuja baada ya maraisi kutoka Colombia, Mexico,Uruguay na Marekani kushauri kuwa bangi itumike kisheria hosipitalini kutibu maradhi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

.