Wednesday 13 August 2014

NAMNA KUJITIBU MAFUA



Mafua ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya mafua na uambatana na homa kali, kutojiskia vizuri, maumivu ya kichwa na dalili nyingi ambazo humfanya mtu kukosa nguvu. yafuatayo ni mambo unayoweza kufanya nyumbani ili kujitibu ugonjwa huu ila usikose kwenda hosipitali kama yote yatashindikana au mafua yanaambatana na dalili nyingine kama kikohozi au kutokupona kwa muda mrefu.


  • Unaweza kunywa dawa baridi kama piritoni, codeine na cetrizene  itakayoweza kufungua pua lililoziba na kuumwa na kichwa.
  • Pua likifura na kuwa jekundu paka mafuta ya Vaseline.
  • Tia puani mwako maji ya chumvi ili kuondoa hali ya kukauka inayotokea wakati ambapo unatumia dawa baridi
  • Ili kukabiliana na koo linalowasha, tumia dawa ya kutibu kikohozi pamoja na asali.
  • Kunywa vitu vioevu Kama maji Safi, ama vinywaji ambavyo havina pombe ili kusafisha mwili wako.
  • Pumzika vya kutosha.
  • Oga maji au osha pua kwa maji ya moto itasaidia kufungua na kulainisha njia ya hewa.
  •  Fanya mazoezi na usipende kukaa ndani au kupumzika muda mrefu
  • Kunywa chai ya moto.
  • Epuka vitu vya baridi kama maji, barafu na ice cream
  • Kula vyakula vyenye uwezo wa kuzuia mafua kama ndizi, pilipili, machungwa, karoti na vitunguu, 

No comments:

Post a Comment

.