Saturday 23 August 2014

TATIZO LA KUUMA NA KUSAGA MENO KWA WATOTO WADOGO.

Watafiti wengi wameshindwa kubainisha dhahiri nini usababisha mtu kutafuna au kuuma meno usiku ili inahusishwa sana na minyoo, maambukizi katika meno na masikio, hasira na msongo wa mawazo kwa yaliyotokea siku nzima, mgangilio mbovu wa meno.
Hii utokea mara nyingi kwa watoto na uweza kusabisha maumivu makali ya taya, kichwa na kuharibika kwa mpangilio wa meno.
 NINI CHA KUFANYA.
Wasiliana na wataalamu wa afya na magonjwa ya meno ili kutibu uwezekano wa kuwepo kwa maambukizi ya minyoo au mfumo wa chakula na upumuaji
Mpunguzie mwanao hasira na mawazo kabla ya kulala kwa kumfanyia vitu vinavyomfurahisha, kumuogesha, kumkanda, kumwimbia nyimbo nzuri, na kumnyoosha misuli.
Mpe chakula bora na maji mengi kwani kuishiwa na maji mwili pia umsababishia maumivu yanayosababisha kusaga meno usiku.
Usimpe vyakula vyenye caffeine kama Kola, Chokoleti, na kahawa kabla ya kulala.
Mzuie kutafuna karamu au vitu vingine wakati mara nyingi wakati wa mchana kwani itajenga mazoea ya kutafna tafna ovyo usiku.
 



No comments:

Post a Comment

.