Tuesday 30 September 2014

FAHAMU KUHUSU KUVIMBA KWA BANDAMA(Splenomegaly)

Maambukizi na magonjwa mengi kwa muda mrefu husabisha kuvimba kwa bandama(spleen)  ambayo iko kushoto mwa tumbo na hivyo kuharibu utendaji wake wa kazi kama kuondoa vimelea kwenye damu, kutengeneza kinga ya mwili, kuondoa chembe nyekundu zisizo na matumizi mwilini. Ugonjwa huu usababishwa na maambukizi ya virusi, vimelea, bakteria, saratani ya damu, presha, magonjwa ya moyo, ugonjwa sugu wa ini, homa ya ini, upungufu wa damu n.k. Tatizo ili lisipotibiwa husababisaha maambukizi na magonjwa ya mara kwa mara, kuvuja damu na kupasuka kwa bandama.

WATU ZAIDI YA 27O WALAZWA KWA KUNYWA TONGWA SONGEA.

Watu zaidi ya 270 wa Kijiji cha Litapwasi, Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma wamelazwa wengi wao wakiwa na hali mbaya katika Zahanati ya Lyangweni na Hospitali ya Misheni ya St Joseph, Peramiho baada ya kunywa togwa inayosadikiwa kuwa na sumu.

RAILA ODINGA ALIVYOSHAMBULIWA KWA KIBOKO.

Hali ya taharuki iliibuka katika mkutano wa hadhara katika jimbo la Kwale nchini Kenya, baada ya mwanamume mmoja kwenda ukumbini na kuanza kumchapa kwa kiboko kiongozi wa upinzani Raila Odinga pamoja na wanasiasa wengine.

Monday 29 September 2014

MBOGA ZA MAJANI NA MATUNDA NI KINGA YA UGONJWA WA KUPOOZA.

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Moyo Marekani (American Heart Association) unaonyesha kuwa mboga za majani na matunda ni kinga sahihi ya kumwondoa binadamu kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa kupooza.

JINSI UNVYOWEZA KUPATA UGONJWA WA NGIRI (HEARNIA)

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Sunday 28 September 2014

POMBE, BANGI, NDOA NA MALARIA CHANZO CHA MAGONJWA YA AKILI.

Inatokea baadhi ya mikoa kuonekana kama ina idadi kubwa ya wagonjwa wa akili kuliko mikoa mingine wapo wanaohusisha wagonjwa hao wa akili na imani za kishirikina pengine bila kujua chanzo kinachopelekea maradhi hayo kutokea.

MADHARA YA MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO(U.T.I) KWA MUDA MREFU.

Kuna madhara mengi yanayosababishwa na maambukizi katika njia ya mkojo au U.T.I kwa muda mrefu. Haya ni baadhi ya madhara hayo na unaweza kuyaepuka kwa kwenda hosipitali na kutibiwa au kubadili mfumo wa maisha.

JITIBU UGONJWA WA MAWE KATIKA MFUKO WA NYONGO(Gallstones).

Ugonjwa huu unasabishwa na kuwepo au kutengenezwa kwa aina ya mawe katika kibofu au mfuko wa nyongo. Tatizo hilo linaonekana kuongezeka kwa kasi katika nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania, lakini linazisumbua zaidi nchi zilizoendela
Gallstones huwapata zaidi wanawake kuliko wanaume na zaidi walio na uzito mkubwa, wanene kupita kiasi wenye umri kati ya miaka 40 hadi 50 hivi.

Saturday 27 September 2014

ORODHA YA MADAKTARI WALIOPATA UFADHILI.

Katibu mkuu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii anawatangazia wafuatao kuwa wamepata ufadhili wa kugharamiwa mafunzo yao ya uzamili/uzamivu kwa mwaka wa masomo 2014/2015. 
BOFYA HAPA KUSOMA MAJINA HAYO.

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO.

 SOMA NA VYAKULA VINAVYOFAA KWA MTU MWENYE VIDONDA VYA TUMBO.

Dalili za vidonda vya tumbo ni pamoja na maumivu makali au kiungulia maeneo ya chembe moyo (epigastic pains): Maumivu juu kidogo ya tumbo mara nyingi huendana na muda wa kula chakula. Mtu mwenye vidonda kwenye tumbo (gastric ulcers) hupata maumivu makali sana kipindi anapokula au mara tu baada ya kumaliza kula wakati aliye na vidonda kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenal ulcers) hupata maumivu makali anapokuwa na njaa na hupata nafuu pindi anapokula. Dalili nyingine ni pamoja na:-

Friday 26 September 2014

TCU YAKIFUNGIA CHUO KIKUU CHA AFYA IMTU KUDAHIRI WANAFUNZI WAPYA.

Tume ya vyuo vikuu nchini Tanzania imesitisha udahili wa wanafunzi wapya katika chuo kikuu cha IMTU kwa mwaka wa masomo 2014/15 na kukipa muda wa miezi 3 chuo hiko kurekebisha kasoro zinazojitokeza mara kwa mara ikiwemo kudahili wanafunzi wengi.

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo Kaimu katibu mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Prof. Magishi Mgasa amezitaja kasoro nyingine zilizopelekea tume hiyo kukifungia udahili chuo hicho ni pamoja na kuendesha program ya ngazi ya cheti bila ya ithbati ya TCU sambamba na kukaidi agizo lilitolewa na Tume hiyo la kusitisha programu hiyo

Amesema katika kipindi cha miezi mitatu ambacho chuo hicho kitakuwa kimesimamishwa kufanya shughuli za udahili TCU itakuwa ikikifuatilia kwa karibu kuona iwapo chuo hicho kitatekeleza na kufuata taratibu zinazotakiwa.

KAMA UNAOTA NDOTO MBAYA HIZI NDIZO SABABU NA TIBA.

Watu wengi husumbuliwa na tatizo la kuota ndoto mbaya usiku ambazo husababisha kujiskia vibaya, hasira na hofu iliyopitiliza. Tatizo ili sio la kuogopa ila huleta shida pale zinapomsababishia mtu kukosa usingizi, kushutuka usingizini usiku, kutokwa jasho na kuogopa kwenda kulala.

TATIZO LA KUTOKWA NA UCHAFU UKENI NA JINSI YA KUJITIBU.


Hakika mapenzi ni matamu hakuna asiyelifahamu hili na mapenzi kwa kawaida hushirikisha vishiriki ngono kama kupapasana, kubusiana na hata mambo fulani ya kula koni na kuzama chumvini. Hakika uke ni sehemu muhimu sana ya mwanamke inayoweza kuamsha hisia za mwanamme wake ama kuzipoteza,kumthaminisha ama kumshusha dhamani endapo mwanamke atashindwa kujiweka katika hali ya usafi ama kukabiliana na matatizo ya kutokwa na uchafu ukeni. Hivyop kwa kutambua hili leo nimeamua kuandika mada hii ili kuwasaidia wale wote wenye tatizo kama hili.....

KAMA UNASUMBULIWA NA KICHOMI.

VIJANA wengi leo nyumbani Bongo wanapatwa na maradhi ambayo zamani yalikuwa ya wazee au watu wa makamo. Maradhi haya ni kama kisukari na mstuko wa moyo.
Kichomi ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya. Ukipatwa muda mrefu au kila wakti ; basi …chunguza zaidi.
Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa.

Wednesday 24 September 2014

KAMA UNASUMBULIWA NA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KULA.

Kukosa hamu ya kula husababishwa na mambo mengi kiafya hasa uchovu uliokithiri, kushiba kupita kiasi, madawa ya kulevya, wasiwasi, hofu, mawazo, majonzi, ulevi, magonjwa na saratani.  Hali hii inaweza kusababisha kukonda na kupungua uzito pamoja na kushuka kwa kinga ya mwili hivyo kushambuliwa na maradhi.
Pamoja na kuwepo na tiba ambazo hutolewa hosipitali sambamba na mazoezi tatizo ili linaweza tibiwa kwa kutumia vyakula vifuatavyo:-

TATIZO LA KUTOKWA NA DAMU NYINGI AU HEDHI ISIYOFIKA KIKOMO.

Menorrhagia ni tatizo la hedhi isiyofikia kikomo zaidi ya siku 7 au kutokwa na damu nzito na iliyoganda kipindi cha hedhi. Hii husababishwa na mabadiliko yasiyo kawaida ya hormoni na matatizo mengine katika njia ya uzazi kama kuumia, maambukizi, saratani, kupungua au kuongezeka uzito kupita kiasi, mawazo na msongo wa mawazo au hasira kupita kiasi.

ONYO: MATUMIZI YA MIRUNGI NI HATARI KWA AFYA YAKO.

Vijana wengi wamejiingiza katika utumiaji wa madawa ya kulevya aina ya mirungi bila kujua madhara yake kiafya.Mirungi ni aina nyingine ya madawa ya kulevya. Mirungi huwa na majina mengine kama vile miraa, mbaga, mogoka, veve, gomba, kashamba. Ingawa imekuwa ni tamaduni kwa nchi za mashariki na saudia Mirungi  huathiri afya yako kwa kusababisha madhara yafuatayo:

EBOLA: WAHUDUMU 6 WASHAMBULIWA KWA MAWE.

Shirikisho la kimataifa la msalaba mwekundu, limesema kuwa kikundi kingine cha wahudumu wa afya kilishambuliwa Jumanne Kusini Mashariki mwa Guinea walipokuwa wanakusanya miili ya watu waliofariki kutokana na Ebola.

Tuesday 23 September 2014

TAMBUA DALILI ZA AWALI ZA SARATANI YA MATITI.

Uonapo dalili hizi wahi hosipitali kwa ajili ya uchunguzi na tiba ya saratani ya matiti mapema.
  • Uvimbe kwenye matiti au kwapa
  • Mabadiliko katika umbo la matiti
  • Chuchu kutoa usaa ama titi kuwa nyororo
  • Chuchu kupotelea ndani ya matiti badala ya kujitokeza nje
  • Madutamaduta kwenye matiti kama yale ya maganda ya machungwa
  • Kubadilika kwa ngozi ya matiti na chuchu kuonekana zimefura

Monday 22 September 2014

MAGONJWA KUMI HATARI USIYOPASWA KUPUUZA.

Mwili wa binadamu huwa na kinga kwa ajili ya kupambana na magonjwa mbalimbali, wakati mwingine kinga hizi hushindwa kufanya kazi kutokana na magonjwa ambayo ni hatari sana hivyo kuitaji tiba au msaada utakaokuwezesha kuishi na ugonjwa huo. Yafuatayo ni magonjwa kumi hatari usiyopaswa kupuuza katika maisha.

JINSI YA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO (U.T.I)

Ugonjwa katika njia ya mkojo (U.T.I) ni ugonjwa unaoshambulia njia za mkojo na husipotibiwa au kuchukuliwa tahadhari mapeme huweza pia kushambulia kibofu na figo hatimaye kuleta madhara zaidi. Ugonjwa huu hutimbiwa kwa kutumia mchanganyiko wa  dawa tofauti ambazo hutolewa kwa ushauri wa daktari. Ili kuepuka ghalama na usumbufu unaosababishwa na ugonjwa huu unaweza kuzingatia mambo yafuatayo ili huweze kujikinga na kuzuia ugonjwa huu.

Sunday 21 September 2014

Saturday 20 September 2014

NJIA RAHISI ZA KUEPUKA NA KUPAMBANA NA MAGONJWA YA MOYO.

Pamoja na magonjwa ya moyo kuwa chanzo kikuu cha vifo vingi duniani kuna uwezekano mkubwa wa kuyaepuka au kuishi nayo salama kwa kubadili mfumo wa maisha tunayoishi. Hizi ni baadhi ya njia unazoweza kutumia kupunguza magonjwa haya:

Friday 19 September 2014

KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI KWA WANAWAKE

Matatizo ya mirija ya uzazi kwa wanawake yapo wengi, mfano mirija inaweza kuvimba na kupoteza uhalisia hivyo kushindwa kutungisha mimba. Mirija inaweza kujaa usaha au maji. Tatizo hili ni kubwa lakini ukifuatilia utakuta linaweza kuzuilika.
Kuziba kwa mirija ni athari za matatizo katika kizazi.

VYAKULA VINAVYOFAA KWA MGONJWA WA KISUKARI

Kisukari ni ugonjwa sugu ambao huathiri uwezo wa mwili kutumia nguvu na chakula kwa muda mrefu kutokana na kuongezeka kwa sukari aina ya glucose kwenye mishipa ya damu. Hii hutokana na mwili kushindwa kutengeneza hormoni ya insulini au kushindwa kutumia insulini iliyopo mwilini ambayo husaidia kupunguza sukari kwenye damu na kuwezesha matumizi yake. Kiasi kikubwa cha sukari kwenye damu huathiri mishipa midogo ya damu kwenye figo, miguu, moyo, macho na mfumo wa fahamu na hatimaye kusababisha kifo. 

KAMA UNASUMBULIWA NA TATIZO LA MIGUU KUTOA HARUFU MBAYA


Miguu kutoa harufu mbaya ni tatizo sugu linalowakabili baadhi ya watu katika jamii, wengi wakiwa wanaume. Tatizo hili linaonekana kuzidi kuwa sugu, hali inayosababisha kuwepo na harufu mbaya hasa kwenye mikusanyiko na wengi wao huwa wagumu kukubaliana na hali yao hata kutafuta tiba mahususi inaweza kuwaondolea kero hiyo.

Thursday 18 September 2014

MADHARA YA SIGARA KWA AFYA YAKO


Kuvuta sigara ni tabia ambayo imezoeleka na watu wengi ingawa ina madhara mengi Uvutaji sigara huathiri mwili kwa njia tofauti na madhara yake ni makubwa kiafya. Inakadiriwa kuwa, hadi sasa kumegunduliwa kemikali zipatazo 7,000 katika moshi wa sigara ambapo 250 kati ya hizo ni sumu na 70 zinasababisha kansa. 

RAMANI KUONYESHA CHANZO CHA EBOLA KUTOKA KWA MNYAMA ANAYESADIKIWA KUWA NI POPO.

Wanasayansi wa chuo kikuu cha Oxford wameonyesha ramani ya maeneo ambako wanyama huenda wana maambukizo ya virusi vya ebola, ikiwa ni hatua ya kwanza kutabiri wapi ugonjwa huu utazuka hapo baadaye.

 Wasanyansi wanasema kuzuka kwa ebola huko Afrika Magharibi kulianza wakati mtu mmoja alipokabiliana na mnyama aliyeambukizwa virusi hivyo. Pengine mnyama huyo huenda akawa ni popo. Wanaweza kuwa na virusi hivyo bila ya kuugua.

KUTANA NA MUUGUZI ALIYEPONA EBOLA NA ANAWASIDIA WAGONJWA WENGINE

Will Pooley ni muuguzi aliyepona virusi vya Ebola baada ya kutibiwa  katika hosipitali ya Royal kusini mwa jiji la London kwa muda wa wiki mbili. Muuguzi huyu anategemea kusafiri kwenda Marekani kwa ajili ya kuwasaidia wahathirika wa Ebola kwa kujitolea damu ambayo inasadikiwa kuwa tayari ina kinga dhidi ya virusi hivi.
CHANZO:BBC

CHANZO, KINGA NA TIBA YA HOMA YA MANJANO (Jaundice)

Homa ya manjano ni tatizo linaosababisha ngozi yako, midomo na sehemu nyeupe ya jicho kuwa ya njano kutokana na kuongezeka kwa rangi ya bilirubini katika damu inayotengenezwa kwenye ini baada ya kuvunjwa kwa seli nyekundu za damu. Hali hii inaweza kuambatana na kinyesi cheye rangi ya udongo mfinyanzi au kutoa mkojo mweusi, mwili kuwasha, kutapika kukosa hamu ya kula na uchovu. 

Wednesday 17 September 2014

KUHUSU MWANAFUNZI ALIYEJINYONGA KWA KUKOSA MATIBABU MKOANI KAGERA

Mwanafunzi wa kidato cha 5 shule ya sekondari Ihungo Ezera Gerald (19) Ameamua kujinyonga kwa kutumia shuka lake katika hospital ya mkoa wa Kagera baada ya kulazwa hospitalini hapo bila kupata huduma na kuacha ujumbe akisema si halali kwa mwanadamu kutibiwa kama mnyama.
Kutokana na tukio ili la kusikitisha unahisi nani alaumiwe na unajifunza nini? Tupe maoni yako kupitia FACEBOOK
Chanzo: ITV

UNAWEZA KUEPUKA MADHARA YANAYOSABABISHWA NA UNENE KUPITA KIAS (Obesity)



Unene kupita kiasi husababishwa kuwa na  mafuta mengi  mwilini kutokana na  kukosa mazoezi ya kutosha au kula chakula kupita kiasi ambacho ukosa matumizi na kuifadhiwa kwenye tumbo, makalio, maziwa au kiungo chochote laini. Hii pia inaweza kuchangiwa na mabadiliko ya hormone asa kipindi cha ujana, uzeeni au ujauzito na kurithi katika familia.

Tuesday 16 September 2014

FAIDA AZIPATAZO MAMA ANAYEMNYONYESHA MTOTO


Miezi sita ya kwanza katika maisha ya mtoto mchanga chakula pekee ambacho wataalamu wa afya wanashauri apewe ni maziwa ya mama tu. Kunyonyesha ndio njia ya kwanza kabisa kumpa mtoto chakula. Unapoanza kumpa mtoto vitu vingine kama maziwa ya kopo wakati ana miezi michache utoaji wako wa maziwa unaathirika maana jinsi mtoto anavyonyonya ndivyo jinsi maziwa yanavyotengenezwa ndio maana watu wengi wanavyoanza kazi na kumuacha mtoto nyumbani maziwa yao yanaanza kupungua. Faida za kunyonyesha maziwa ya mama ni pamoja na:

TAHADHARI KWA WANAUME WANAOWATELEKEZA WATOTO.

Tahadhari kwa wanaume wanaowatelekeza watoto wao nchini Kenya.Baadhi tayari wameanza kupata tumbo joto.
Kikundi cha wanaume watatu nchini Kenya kimezindua ukurasa wa Facebook ambao lengo lake ni kuwajibisha wanaume wasiotekeleza majukumu yao ya kuwalea watoto wao.Mtandao huo unaitwa Deadbeat Kenya.
Mtandao huo tayari umepata mashabiki wengi sana huku baadhi ya wale walioaibishwa wekiwemo wanasiasa, wanamuziki na watu mashuhuri.

SABABU NA TIBA YA TUMBO KUJAA GESI.

Tatizo la tumbo kujaa gesi husababishwa  na kumeza chakula pamoja na gesi inayotolewa katika vyakula mbalimbali tunavokula ambayo hujaa tumboni na kwenye utumbo mdogo. Hali hii husababisha tumbo kujaa au kuvimba na mtu hutoa gesi hiyo kwa njia ya ushuzi na kubeua.

SOMA KUHUSU SAMAKI ALIYEFANYIWA UPASUAJI WA UBONGO.

Samaki aina ya Goldfish,
anaendelea kupata nafuu baada ya
kufanyiwa upasuaji kutolewa
uvimbe kwenye ubongo wake.
Upasuaji huo umesemekana
kufanywa kwa uangalifu mkubwa
kutokana na hofu yatisho kwa
maisha ya Samaki huyo.
Samaki huyo kwa jina George,
ambaye mmiliki wake anaishi
Melbourne, alidunguwa sindano ya
kuondoa fahamu iliyogharimu dola
200.

MADHARA YA KUTOBOA PUA, MDOMO NA ULIMI

Katika zama hizi za utandawazi na muingiliano baina ya tamaduni zetu za asili na tamaduni za kimagharibi, imekuwa ni kawaida kwa vijana wa rika tofauti na jinsia zote kutoga ulimi, mdomo, kitovu ama kivimbe cha nyusi kwa sababu tofauti tofauti sana. Hivyo basi, ni muhimu sana kufahama ukweli kuhusu faida ama hasara za kutoga ulimi ama mdomo kabla hujatekeleza azma yako ya kutoga viungo hivi vya mwili.

Monday 15 September 2014

ZIJUE FAIDA KUMI ZA ASALI KIAFYA.


Kwa miaka mingi asali imekuwa ikitumika kiafya kwa ajili ya tiba asili ya magonjwa na matatizo mbali mbali kama maambukizi, kuungua, vidonda, makovu, uvimbe na maumivu. Zifuatazo ni faida kumi za asali kiafya:-

FAHAMU KUHUSU DALILI NA TIBA YA SARATANI YA DAMU(Leukemia)

Leukemia ni Saratani ya damu ambayo huanzia kwenye mafuta au urojo wa mifupa na kusababisha uzalishaji wa chembe hai za damu zisizo kawaida kwa wingi na kusababisha upungufu wa damu, kuvuja damu na mwili kushindwa kupigana na maambukizi mbali mbali. Saratani hii hauambukizwi bali hurithiwa kutokana na  mabadiliko katika DNA ambayo huathiriwa na mionzi mikali, maambukizi ya virusi, kemikali hatari na matumizi ya tumbaku na sigara kwa muda mrefu.
DALILI NA ISHARA 
Uvimbe shingoni, kwapani, sehemu ya kushoto ya tumbo na shemu za siri
Kutokwa na damu mara kwa mara puani, sehemu ya haja kubwa, na damu nyingi wakati wa hedhi
Homa za mara kwa mara na kutokwa jasho sana usiku
Maumivu ya mifupa
Kukosa hamu ya kula na kupungua sana uzito
Uchovu wa mara kwa mara
Michubuko na majeraha mengi kwenye mwili
TIBAYA UGONJWA HUU.
Matibabu ya saratani hii hutegemea aina ya saratani, kusambaa kwa saratani., umri na matibabu ya awali ambayo uhusisha dawa, mionzi, kuongezewa damu na kupandikiza. Tiba hizi huwa ni kwa ajili ya kupunguza dalili, kuua chembe hai zisizo kawaida na kuongeza kinga ya mwili.
 JINSI YA KUKABILIANA NA UGONJWA HUU.
Kula lishe yenye mboga za majani na matunda itasaidia kukinga mwili na magonjwa na kuongeza damu.
Tumia mafuta ya samaki yana omega-3 fatty acid ambayo huzuia uzalishaji  wa chembe za damu zisizo kawaida kwa wingi na kuruhusu zile za kawaida kwa ajili ya kulinda mwili.
Pata chanjo za mara kwa mara ili kuzuia maambukizi kwani saratani hii huvutia sana maambukizi kutokana na kushusha kinga ya mwili.
Fanya mazoezi mepesi mara kwa mara.
Pata msaada kutoka kwa wataalamu wa afya, ndugu jamaa na marafiki na usiwe mpweke muda mwingi.
Kunywa juisi glass moja kila asubuhi itasaidia kuimarisha mwili na kuongeza kinga.
Epuka matumizi ya pombe, sigara na tumbaku.
Kumbuka ugonjwa huu ni hatari hivyo jamii inabidi ichukue tahadhari kubwa, kwani inaelekea jamii haina kabisa uelewa wa ugonjwa huu na jinsi ya kukabiliana nao.
LIKE PAGE NA WASILIANA NASI FACEBOOK KWA MSAADA ZAIDI 



Sunday 14 September 2014

SABABU ZA WATOTO WADOGO KULIA NA JINSI YA KUWABEMBELEZA

Kama mzazi mpya, wakati mwingine inakuwa vigumu kutambua mtoto wako anahitaji nini anapolia. Mzazi anaweza kuwa na maswali kadhaa kichwani mwake, je, mtoto ana njaa, anasikia baridi, ana kiu, anaumwa ama amechoka? Katika siku za mwanzo, hali ya namna hii inawawia vigumu wazazi wengi, wasijue nini la kufanya. Hata hivyo, kwa kadiri siku zinavyopita mzazi mpya ataweza kutambua kuwa kilio cha mtoto wake kinamaanisha anahitaji nini kutokana na mfumo wake wa kulia.

KUHUSU UGONJWA WA KASWENDE (Syphilis)

Ugonjwa huu nao husababishwa na bacteria Treponema Pallidum
Dalili zake hazionekani kwa urahisi. Huenda ukaanza kwa kijidonda au kipele kwenye uke au uume au sehemu ya kupitishia haja kubwa. Kidonda hiki kinapopona usidhani ndio mwisho wa maambukizo la! Viini hivyo vinaweza kubaki mwilini kimya kimya kwa miaka mingi!

Saturday 13 September 2014

DALILI NA TIBA YA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.

Upungufu wa mbegu za kiume uchangiwa na kurithi magonjwa mbalimbali yanayoathiri mirija ya uzazi,  korodani na upungufu wa hormoni ya kiume (testosterone), kuumia kwa korodani, joto na unene kupita kiasi, ukosefu wa lishe asa zenye zinc, selium na vitamin C na D, kuvaa nguo za kubana muda mrefu, uvutaji wa sigara unyaji wa pombe na matumizi ya madawa kupita kiasi, unene kupita kiasi, maambukizi ya zinaa kwa muda mrefu, msongo wa mawazo na athari za mazingira kama sumu na mionzi.

FAHAMU KUHUSU DALILI, MADHARA NA TIBA YA KISONONO AU GONO



Kisonono ni ugonjwa wa zinaa unaoambukizwa, ugonjwa huu hutokana na wadudu aina ya Neisseria gonorrhoeae. Ugonjwa huu pia huambukizwa kwa tendo la ngono na hata kutoka kwa mama mjamzito anapojifungua huweza kumuambukiza pia mtoto endapo atakuwa alikuwa nao.

Friday 12 September 2014

MADHARA YA KUKOROMA USIKU NA TIBA YAKE.

Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala ambalo linaweza kuwatokea watu wa kila umri ingawa hutokea mara nyingi kwa wanaume au watu wanene. Kukoroma huzidi kwa kadri umri unavyoongezeka na asilimia 54 ya watu wazima hukoroma baadhi ya wakati huku asilimia 25 ya wengine wakiwa na tabia ya kukoroma kila wakati. Kukoroma baadhi ya wakati kwa kawaida sio tatizo kubwa na mara nyingi huleta tu karaha kwa mtu anayelala karibu na mkoromaji. Hata hivyo kukoroma huko sio tu kwamba huharibu usingizi wa anayekoroma bali pia huwasumbua na kuwakeresha wanaolala karibu na mkoromaji. Wale wenye tabia ya kukoroma, hukoroma kila wanapolala na mara nyingi huchoka wanapoamka, na watu wa aina hii hushauriwa kumuona daktari na kushauriwa kuhusiana na tatizo hilo. Lakini kabla hatujaendela mbele ni bora tujue kukoroma hasa ni nini au hutokea vipi?

MAMBO KUMI MUHIMU KATIKA KUDUMISHA MAHUSIANO.



Watu wengi wamekuwa katika hali ya kutafta na kujenga uhsiano wa muda mrefu lakini hushindwa kufanikiwa kutokana na kushindwa au kupuuza vitu vidogo mbele ya wapenzi wao na kushindwa kutambua kuwa mapenzi hayajengwi kwa kutumia nguvu na pesa bali kwa kufanya yafuatayo.

NJIA ZA KUPUNGUZA NA KUZUIA MAUMIVU YA KICHWA.

Maumivu ya kichwa hutokea sehemu yoyote ya kichwa na hutokana na itilafu katika misuli,mishipa ya damu na fahamu au viungo vyovyote vinavyozunguka ubongo. Mara nyingi maumivu haya huwa sio hatari sana japo humkosesha mtu raha. maumivu haya kuzuiwa na kupunguzwa kwa kufanya mambo yafuatayo kabla ya kwenda hospitali maumivu yanapozidi.

MAZOEZI YATAKAYOKUSAIDIA KUFAULU MITIHANI

Tafiti zinaonesha kuwa mazoezi ya kutembea, kuendesha baiskeli, kusoma vitabu, chemsha bongo, michezo ya uwanjani, tv na kompyuta husaidia sana katika ufaulu wa mitihani kwa wanafunzi kwa kuongeza akili ya kufikiria haraka na utunzaji wa kumbukumbu kichwani.
BOFYA HAPA KUUNGANA NASI FACEBOOK USIPITWE NA MENGI ZAIDI.

Thursday 11 September 2014

UNAWEZA KUMUHUDUMIA MGONJWA WA KIFAFA.

Utendaji mzuri wa ubongo unategemea uwiano katika kutuma ujumbe. Utumaji usio na udhibiti hupelekea mlipuko wa umeme katika seli za ubongo ambapo huweza kupelekea mtu kupata kifafa (seizure) hali ambayo huambatana na kupoteza fahamu,kuzubaa,kukakamaamisuli, kuchanganyikiwa, kutokwa na haja ndogo au kuchezesha viungo haswa mikono na miguu.

UPUNGUFU WA DAMU KWA WAJAWAZITO (Anemia in Pregnancy)

Upungufu wa damu (anaemia) hutafsiriwa kama kupungua kwa kiwango cha hemoglobin katika damu damu chini ya kiwango kinachokubalika kiafya. Kiwango cha kawaida cha haemoglobin (Hb) katika mwili wa binadamu ni kati ya gramu 12 mpaka 14 kwa kila mililita ya damu. Hata hivyo shirika la afya duniani (WHO) linatambua kiwango cha mpaka 11gm/mililita kuwa cha kawaida kwa mama mjamzito. Hivyo basi mjamzito mwenye kiwango chochote cha haemoglobin chini ya 11 gm/mililita hutafsiriwa kuwa na upungufu wa damu. Hata hivyo nchi nyingi hasa zinazoendelea hutambua kiwango cha mpaka gramu 10 kwa mililita kuwa ni upungufu wa damu kwa mjamzito.

.