Madaktari na wataalamu wa afya wanashauri mama
mjamzito kufanya mazoezi mepesi kwa muda wa dakika 10 mpaka 30 kila siku
ili kuimarisha misuli, mzunguko wa damu, viungo vya uzazi na kupunguza
uzito. Zifuatazo ni faida anazozipata mama mjamzito iwapo atafanya
mazoezi
1. Mazoezi hupunguza maumivu ya kichwa, kukosa choo na kuvimba mwili.
2. Mazoezi huongeza nguvu na kuupa mwili stamina.
3. Mazoezi hukufanya ujisikie vizuri na kukufanya uwe katika hali ya furaha.
4.
Mazoezi hupunguza maumivu ya mgongo na huimarisha mifupa ya mgongo,
makalio na mapaja na kuifanya iwe na uwezo wa kuvumulia vyema uzito wa
mimba.
5. Mazoezi husaidia huongeza mtiririko wa damu na hewa katika ngozi na kuifanya ngozi yako ionekane nzuri.
6. Mazoezi hutayarisha mwili wako uwe tayari kwa ajili ya kuhisi uchungu kwa muda mfupi na kujifungua kwa urahisi.
7. Mazoezi hufanya mwili wako urudi upesi katika muonekano wake wa kawaida baada ya kujifungua.
8. Mazoezi humsaidia mama mjamzito apate usingizi kwa wepesi na kulala vyema.
10. Huongeza hisia, usingizi na kupunguza maumivu ya viungo
No comments:
Post a Comment